KULIA NI CAPT.SAMBWEE SHITAMBALA WAKATI ANARUDI CCM AKIKUMBATIANA NA RAIS JAKAYA KIKWETE (Picha Maktaba).
NA SOLOMON MWANSELE,KYELA
MJUMBE wa halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), ya CCM, Sambwee
Shitambala, amesema watanzania hawana utamaduni wa kuvipenda vyama vyenye lengo
la kutaka kuigawa nchi katika vipande.
Imeelezwa wakati CCM imekuwa kila mara ikiongelea umoja na
mshikamano miongoni mwa watanzania, CHADEMA wao wanataka kuigawa nchi kwa
kuanzisha mfumo wa majimbo.
Shitambala aliyasema hayo jana wakati akihutubia mamia ya
wananchi wa wilaya ya Kyela, waliojitokeza katika maadhimisho ya miaka 36 ya
kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wilayani humo.
Alisema uhuru, umoja na mshikamano ndiyo misingi ya CCM,
tofauti na CHADEMA ambao mara zote wao wamekuwa mabingwa ya kuwahamasisha na
kuwashawishi wananchi kuandamana, kuchoma barabara na kufanya vurugu zisizo na
msingi.
“Tunahitaji kuendelea kuwa na Tanzania moja, lakini wenzetu wa
CHADEMA wao wanataka kuigawa nchi katika majimbo.Watanzania hatupendi vyama
vyenye lengo la kuigawa nchi yetu kimajimbo” alisema Shitambala na
kushangiliwa.
Aliongeza CCM kupitia serikali zake, kimeleta maendeleo
mengi na yanayoonekana wazi kwa watanzania, hivyo kuwataka wananchi wa wilaya
ya Kyela na watanzania kwa jumla, kuwapuuza wanaaiasa wanaosema hakuna
lililofanyika tangu nchi ipate uhuru 1961.
Mjumbe huyo wa NEC alisema hakuna serikali yoyote duniani,
inayoweza kuwajaza wananchi wake fedha mifukoni, hivyo kutoa rai kwa wana-Kyela
wawe makini na kamwe wasikubali kuchuuzwa na wanasiasa uchwara.
Alisema CCM imekuwa inasimamia vyema ugawaji na usimamizi makini
wa rasilimali za Taifa letu, tofauti na CHADEMA ambao wao kupitia sera yao ya majimbo, wanataka
kila mkoa unufaike na rasilimali zake badala ya Taifa zima.
Shitambala alisema vile vile CCM imekuwa na demokrasia ya
kweli kwa viongozi wake kuchaguliwa kwa kura na wananchi, tofauti na CHADEMA
ambao wamekuwa wanagawana uongozi kwa kutanguliza undugu, urafiki na ukabila.
“Mimi sijawahi kuwa mpinzani bali nilienda CHADEMA kuangalia
jinsi wanavyoendesha siasa zao kwa kutanguliza ukabila… napenda kuitumikia nchi
yangu, ndiyo maana nilipoona wanataka kunitumia kuendesha mikutano ya vurugu
niliwakimbi na kurudi CCM” alisema Shitambala.
Aliongeza CCM kinataka watu wachape kazi kwa bidii na
maarifa kwa lengo a kuinua vipato vyao na ndiyo maana licha ya sikukuu ya
kuzaliwa kwake (Februali 5, ya kila mwaka), iliangukia siku za kazi, lakini kwa
busara za hali ya juu kiliamua kurudisha nyuma sherehe zake.
Shitambala
alisema CCM haikudondoka kama Uyoga kama vilivyo
vyama vingine vya siasa nchini, na ndiyo maana vyama vingine havina
waasisisi kama ilivyo kwa CCM ambayo ni zao la TANU na Afro Shiraz.
0 comments:
Post a Comment