Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
*Ni baada ya kukamatwa na Uongozi wa Kijiji.
*Chanzo ni Mishikaki ya Shilingi 1,000/=
Mkazi
wa Kitongoji cha Gezaulole, Kijiji cha Haporoto Kata ya Ihango Wilaya
ya Mbeya Vijijini Mkoani Mbeya Mbwiga Mwandele(50 -55) amejinyonga kwa
kutumia mkanda wa Suruali yake katika Ofisi ya kijiji hicho.
Tukio hilo limetokea Oktoba 26 mwaka huu majira ya saa mbili usiku na maiti yake kugunduliwa Oktoba 27 saa mbili asubuhi.
Kwa
mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa marehemu kabla
hajafikwa na mauti alidaiwa deni la shilingi 1000 ambayo inadaiwa kuwa
alikula mishikaki(nyama) eneo la Kilabu cha Kijiji cha Haporoto, ambapo
huuza pombe za kienyeji na marehemu kushindwa kulipia mishikaki na
kupelekwa katika Ofisi ya kijiji.
Aidha
Uongozi wa Kijiji hicho chini ya Mwenyekiti wake Bwana Daimon Mndewa
alimwachia jukumu mgambo wa kijiji hicho Bwana Fredy Wiston, kumlinda
marehemu ili asubuhi ya Oktoba 27 suala hilo lizungumzwe lakini
ilipofika asubuhi mgambo huyo alikuta Mwiga amejinyonga kwa kutumia
mkanda wa suruali aliokuwa ameuvaa marehemu kabla ya kifo chake.
Kwa
upande wake Mke wa marehemu Bi Malita Mbwiga(45) amesema waliachana na
mumewe muda mfupi walipokuwa wakinywa pombe na yeye kuamua kurejea
nyumbani na marehemu hakurejea nyumbani na baadae alipata taarifa ya kuwa kajinyonga katika Ofisi ya kijiji Oktoba 27 mwaka huu majira ya saa mbili asubuhi.
Hata
hivyo Mwenyekiti wa Kitongoji cha Gezaulole Bwna Raphael Jailos Mbenya
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na mwili wa marehemu ulichukuliwa
na jeshi la polisi hadi hospitali ya Rufaa jijini Mbeya na kwamba Jeshi
la polisi linawashikilia Mwenyekiti wa kijiji na mgambo kwa mahojiano na
kwamba wakati wa tukio Afisa Mtendaji wa kijiji Bwana Mwalingo Mbenya
hakuwepo kijijini hapo.
0 comments:
Post a Comment