Mkunga
wa Jadi Bi Agripina Namwichi(37)(kulia) akimkabidhi mtoto wa kiume Bi
Shija Bundala(26) mkazi wa Kijiji cha Mbuyuni, Wilaya ya Chunya Mkoani
Mbeya mara baada ya kujifungua salama mtoto wa kiume nyumbani kwa mkunga
huyo. Awali mwanamke huyo amewahi kujifungua watoto kwa awamu mbili
kupitia Oparesheni katika Kituo cha Afya cha Mbuyuni lakini kwa mkunga
huyo inadaiwa alijifungua salama salimini licha ya kuwa na uhaba wa
vifaa na eneo maalufu la kitaalamu.
Mkunga akiandaa eneo la akina mama wajawazito kwa ajili ya mapumziko kabla ya kujifungua.
Mkunga
akionyesha vibali vinavyothibitisha ruhusa aliopewa na Serikali kwa
ajili ya kutoa huduma ya kuwazalisha akina mama wajawazito.
Mkunga
Bi Agripina akiangalia orodha maalumu ya watoto waliozaliwa katika
kituo chake,ambapo zaidi ya watoto 187 wamezaliwa kwa mwaka 2012.
Mkunga akionesha kadi za kliniki ambazo hujanazo akina mama na huzikagua kama kuma kasoro zozote.
Chumba maalumu kwa ajili ya kuzalia(labor)
Mandhari
au sehemu ya kupumzikia akina mama wajawazito ambao hufika kwa mkunga
kwaajili ya kujifungua.(Picha zote na Ezekiel Kamanga,Chunya)
NB;-
Changamoto ambazo huwabiliwa nazo ni pamoja kuvuja kwa chumba cha
kuzalia hususani katika msimu wa masika,uhabawa vifaa vya
kuzalishia,vitanda na magodoro na hakuna tozo yoyote ambayo huwadai
akina mama wajawazito.
0 comments:
Post a Comment