Pages


Home » » WATOTO 200 WANAISHI MAZINGIRA HATARISHI RUNGWE

WATOTO 200 WANAISHI MAZINGIRA HATARISHI RUNGWE

Kamanga na Matukio | 03:08 | 0 comments
Na,ANGELICA SULLUSI

Zaidi ya watoto 200 wanaishi katika mazingira magumu katika kituo cha Ndaga Wilayani Rungwe Mkoani hapa kutokana na ukosefu wa mahitaji muhimu ya binadamu.
 
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa mtandao wa wanawake Tanzania (INUKA) ambaye pia ni mwanasheria DAVID MSUYA  wakati akizungumza na Mwandishi wetu.
 
MSUYA amesema kuwa watoto hao zaidi ya 200 ambao ni wa jinsi zote wanazalimika kutumia choo kimoja kwa ajili ya kujisaidia jambo ambalo ni hatari kwa afya zao.
 
Amesema kuwa kituo hicho ambacho kilianzishwa kama sehemu ya ibada kimelazimika kutumika kama kituo cha kulelea watoto yatima kwa kuwa walijikusanya watoto wengi kwa ajili ya kutafuta msaada hivyo hakuna vyumba vya kutosha kuwahifadhi watoto hao.
 
Aidha,ametoa wito kwa taasisi mbalimbali kujitokeza kuwasaidia watoto hao wanaohitaji msaada wa haraka katika kuendesha maisha yao.
 
Kwa upande wake Mchungaji wa Kanisa la Bethel Miracle Center(Kituo Cha Mbinguni) ambalo ndilo limechukua dhamana ya kuwalea watoto hao lililopo Soweto Jijini Mbeya, MCHUNGAJI  JONATHAN KYANDO amesema kuwa kanisa hhilo haliwezi kutosheleza mahitaji ya watoto hao kwani wanategemea sadaka za waumini.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger