*Polisi wajikanyaga mahakamani.
*Watoto wachanganywa mahabusu moja na watu wazima.
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbozi
Mahakama
ya Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya imetakiwa kufuta mashtaka ya kesi ya
jinai namba 143/2012, inayomhusisha Bwana Paulo Sichone na wenzake 12
kutoka Kijiji cha Myunga, Kata ya Myunga Wilaya ya Momba Mkoani hapa.
Kauli
hiyo imetolewa na Wakili anayewatetea washtakiwa Mheshimiwa Edgar
Bantulaki, mbele ya mahakama hiyo kutokana na upande wa mashtaka
kushindwa kuwasilisha jalada la mashtaka kwa zaidi ya siku 62, ambapo ni
kinyume na sheria namba 201 iliyofanyiwa marekebisho na kuwa 225
akitolea mfano wa kesi namba 12/1979 iliyomhusu Deenan Crispin ambapo
mwendesha mashtaka alishindwa kuleza maelezo mahakamani hivyo mshtakiwa
kuachiwa huru.
Kwa
mujibu wa kifungu hicho washtakiwa wanapaswa kuachiwa huru kutokana na
washtakiwa kufikiswa mahakamani huku mwendesha mashtaka akitoa
visingizio mbalimbali hali iliyopelekea washtakiwa hao kuendelea kusota
mahabusu baada ya kuwanyima dhamana.
Mheshimiwa
Wakili Bantulaki ameiambia mahakama hiyo kuwa wateja wake walifikishwa
mahakamani hapo Agosti 13 mwaka huu na mahakama kuahirisha kesi hiyo
hadi Agosti 27 mwaka huu, baada ya Mwendesha mashtaka kudai upelelezi
umekamilika na kuomba Septemba 10 mwaka huu kesi hiyo kusikilizwa,hata
hivyo kesi hiyo kesi hiyo iliahirishwa tena hadi Septemba 2 mwaka huu
kwa madai kuwa jalada la kesi limepelekwa kwa Kamanda wa Jeshi la polisi
mkoa.
Aidha
ilipofika Septemba 24 mwaka huu bado mwendesha mashtaka alitoa
kisingizio cha kuwa jalada hilo halijarejeshwa na kesi kuahirishwa mpaka
Oktoba 2 mwaka huu ambapo pia siku hiyo aliiambia mahakama jalada analo
hivyo anaiomba tena mahakama kupanga tarehe ya kusoma maelezo ya awali
na kupangwa kusikilizwa Oktoba 15 mwaka huu, ambapo siku hiyo mwendesha
mashtaka aliiambia mahakama kuwa jalada halipo hivyo aliiomba tena
mahakama kutaja tarehe nyingine ya kusikiliza kesi.
Hata
hivyo, ombi hilo lilipingwa na wakili anaye watetea washtakiwa na kudai
kuwa kwa mujibu wa sheria kama mwendesha mashtaka ameshindwa
kuwasilisha maelezo kwa kipindi cha siku 60 kesi inapaswa kuondolewa
mahakamani na kwamba hakubaliani na maelezo hayo.
Baada
ya mabishano ya muda mahakamani hapo, mahakama ilitoa siku mbili kwa
upande wa mashtaka kuwasilisha jalada na kama akishindwa basi
atakubaliana na upande wa wakili wa washtakiwa na kupanga kesi hiyo
kusikilizwa Oktoba 18 mwaka huu.
Wakati
huohuo katika hali isiyokuwa ya kawaida watoto wawili wamejumuisha
katika kesi hiyo ambapo wapo chini ya umri wa miaka 18 ambao ni Ezebius
Sinzumwa(15) na Damasi Sinzuma (17) waliochanganywa katika mahabusu ya
watu wazima na kwamba mahakama hiyo haikupaswa kusikiliza shauri hilo
ili mahakama husika ndiyo isikilize.
Pamoja
na ombi la wakili watoto hao bado wanajumuishwa ma watu wazima ambapo
asasi ya haki za binadamu imelaani kitendo hicho kupitia mwenyekiti
wake wa Mkoa Bwana Said Madudu.
0 comments:
Post a Comment