*Adai kuangusha magari 15, auwa watu 15 mpaka sasa.
*Aonesha ngozi ya mtoto wa miaka miwili.
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Mwanamke
aliyejitambulisha kwa jina la Belikumana Lugome(48), Mkazi wa Kijiji
cha Parangu Songea Mkoani Ruvuma amekiri kujihusisha na imani za
kishirikina na kukabidhi sehemu ya madawa aliyokuwa akiyatumia kwa
Mganga wa Jadi aliyefahamika kwa jina la Jesca Ndembo Mkazi wa Iyunga
Mkoani Mbeya.
Mwanamke
huyo alifika kwa Mganga huyo wa jadi Oktoba 12 mwaka huu, majira ya saa
8 mchana alipokwenda hapo kwa nia ya kumwangalia shangazi yake
aliyekuwa akitibiwa na Mganga huyo.
Aidha
imedaiwa kuwa shangazi yake huyo alirogwa na nduguye na mshirikina huyo
kukiri kwamba ndiye alisababisha upasuaji wa tumbo lake mara mbili na
kutakiwa apasuliwe tena na kama asingewahi angeuawa kwa siku za hivi
karibuni.
Bi. Lugome amekiri kujihusisha na matukio ya ajali 15 mkoani Ruvuma na kusababisha vifo vya watu 15 katika ajali hizo.
Aidha alionesha sehemu ya vifaa ambavyo alikuwa akivitumia katika ushirikina ikiwemo ngozi ya mtoto wa miaka miwili.
0 comments:
Post a Comment