Na Ester Macha,
NAIBU
waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Bw.Adam Malima amesema kuwa sababu
kubwa ambayo inayochangia kupoteza viti vya ubunge katika maeneo mbalimbali
nchini ni kutokana na makundi yaliyogawanyika ndani ya chama kipindi cha kura
za maoni ndani ya chama hicho.
Amesema
kuwa makosa ambayo huwa yanafanyika wakati wa kupitisha majina ambapo jina
linalopitishwa linakuwa sio chaguo la wanachama hivyo hulazimika kumpa
mtu yeyote kutokana na chama kuweka jina ambalo halitakiwi kwa wanachama.
Bw. Malima alisema yote inatokana na chama cha mapinduzi kupoteza viti vya
ubunge katika maeneo mbali mbali ni kutokana wagombea walio wengi kukataliwa
kwenye kura za maoni ndani ya chama hicho.
Akitolea
mfano Mkoa wa Iringa alisema kwamba Mbunge wa sasa Mchungaji Msigwa hana uwezo
wa kuwa Mbunge katika jimbo la Iringa bali wananchi walilazimika kumchagua
kutokana na kura za maoni ndani ya ccm katika kumchakato wa kumchagua
mgombea wa Ubunge wa jimbo hilo..
Bw.
Malima alisema hayo jana wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa
chama cha mapinduzi uliofanyika katika viwanja vya sokoine Jijini hapa.
“Mfano
tosha tunao kutoka Mkoa wa Iringa jina lililopitishwa ndani ya halmashauri kuu
ya CCM halikuwa chaguo la wanachama hivyo wananchi wote
wakalazimika kumchagua Mbunge ambaye hakupaswa kuwa mbunge “alisema Bw. malima.
Akizungumzia
kwa Mkoa wa Mbeya alisema kuwa kwamba kwa kawaida Mbeya ni ya chama cha
mapinduzi lakini katika uchaguzi uliopita walijikwaa ndio maana ilifika mahala
wakapoteza viti viwili vya ubunge ambavyo ni Mbeya Mjini na Mbozi
Magharibi.
Alisema
kuwa hata Mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Bw.Mbilinyi nae hana uwezo wa kuingia
bungeni na kuwatetea wananchi wake hali kadhalika na Mbozi magharibi pia hawafanani
na wananchi wanaowaongoza ambao wanatakiwa kwenda kuwatetea bungeni bali yote
hiyo ilitokana na kujikwaa kwa chama .
Hata
hivyo alisema kwamba katika chaguzi mbali mbali ndani ya chama cha mapinduzi ni
sawa na usajili wa timu ambayo itakayokwenda kushindana mwaka 2015 hivyo makosa
yaliyofanyika kipindi kilichopita inatakiwa kuyarekebisha sasa ili
kuondokana na makundi yasiyokuwa na tija ndani ya chama cha mapinduzi ambayo
yamekuwa yakitoa nafasi ya kushinda kwa vyama vya upinzani .
“Uchaguzi
huu ambao tunafanya leo ni usajili wa timu itakayokwenda kushindana kwenye
uchaguzi wa mwaka 2015 hivyo ni vema tukawa na timu nzuri ambayo itakuwa na
nguvu kubwa na upinzani kushindwa kutumia mianya hiyo ambayo imekuwa ikitoa
nafasi kubwa kwa wapinzani kupenye kwa kutumia makundi yetu ndani ya
chama”alisema Malima.
0 comments:
Post a Comment