Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mh Abbas Kandoro.
Na
Esther Macha, Mbeya
MKUU
wa Mkoa wa Mbeya Bw. Abbas Kandoro ameonya tabia ya baadhi ya watu ambao
wamekuwa wakianzisha vyuo vya Ufundi Stadi kienyeji bila ya kuwa na
usajili wowote kutoka serikalini hali ambayo imekuwa ikirudisha nyuma
maendeleo ya elimu ya ufundi nchini.
Amesema kuwa vyuo vingi vya ufundi
vimekuwa vikianzishwa tu bila kufuata utaratibu wowote na wahusika na hivyo
kusababisha wanafunzi kukosa sifa za kufanya mtihani yao ya mwisho.
Bw. Kandoro aliyasema hayo jana
wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wamiliki wa Vyuo vya ufundi stadi,pamoja
na wakuu wa vyuo vya ufundi stadi na secretariat ya Veta Kanda ambapo
mafunzo hayo yanafanyika katika ukumbi wa mikutao wa veta uliopo chuoni hapo.
“Hali hii inasikitisha sana
ukitembea mitaani huko vyuo vimejazana lakini havina usajili na kwamba hali
hiyo inapoteza muda sana kwa vijana wetu kwani baadaye huambiwa hawana
namba za usajili wakati wa kufanya ,mitihani yao ya mwisho kutokana na kutokuwa
na namba za usajili ambazo zinasababisha vyuo hivyo kuendeshwa bila kufuata
utaratibu na sheria”alisema Mkuu huyo wa Mkoa.
Hata hivyo alisema kuwa kama mkoa
hawana tatizo na watu ambao wanaanzisha vyuo kwani lengo lao ni zuri la
kuhakikisha kuwa kila kijana anapata ajira badala ya kukaa
vijiweni,kikubwa ni kufuata taratibu za serikali ili kuwa na usajili
halali.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema vyuo
vikiwa vingi vitasaidia vijana kuwa na elimu ambayo ni endelevu na kwamba
kupitia ufundi huo vijana wanazpata ujuzi wa ufrundi mbali mbali.
Aidha Bw. Kandoro aliwashauri wazazi
na vijana kuona kuwa elimu ya ufundi stadi ni mchepuo mwingine wa
elimu na sio chaguo la mwisho mara wanapokosa fursa ya
kuendelea na elimu ya sekondari au elimu ya juu.
Alisema wazazi wana wajibu kuweka
kipaumbele elimu ya ufundi kwani ni sawa na elimu nyingine ambazo zimekuwa
zikipewa nafasi .
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Veta
Kanda ya Kusini Magharibi Bw.Justine Rutta alisema maqfunzo hayo yatajumuisha
washiriki kutoka mikoa ya , Mbeya, Rukwa pamoja na Kata na kwamba mkutano huo
utakuwa na washiriki 64 ambao utakuwa na wamiliki wa vyuo vya ufundi
stadi,wadau mbali mbali wa elimu na mafunzo ya ufundi ,wakuu wa
vyuo vya ufundi stadi.
Bw. Rutta alisema kuwa katikia
mafunzo hayo kila chuo kitasoma taarifa fupi ya chuo chake ili kufahamu
mapungufu yaliyopo ,pamoja na miongozo na taratibu za usajili wa vyuo ili
kuwa na vyuo vya ufundi stadi vyenye hadhi bora.
0 comments:
Post a Comment