Na Ester Macha,Mbeya.
MAMLAKA ya majisafi na Usafi wa Mazingira Jiji la Mbeya, imesema kuwa shule za serikali pamoja na jeshi la polisi ndizo zinaongoza kwa kuwa na madeni ya makubwa ya maji kutokana na kutolipwa kwa wakati na hivyo kusababisha mamlaka kuwa na utendaji mgumu wa kazi .
MAMLAKA ya majisafi na Usafi wa Mazingira Jiji la Mbeya, imesema kuwa shule za serikali pamoja na jeshi la polisi ndizo zinaongoza kwa kuwa na madeni ya makubwa ya maji kutokana na kutolipwa kwa wakati na hivyo kusababisha mamlaka kuwa na utendaji mgumu wa kazi .
Kufuatia kuwepo kwa madeni hayo mamlaka
ya maji imeanza opareshemni ya kukata maji kwa maeneo yote ya wananchi
ambako hawajalipa ada.
Kauli hiyo imetolewa jana na Ofisa Uhusiano wa Mamlaka ya
maji Jijini hapa Bibi. Neema Stanton wakati alipozungumza na gazeti hili
ofisini kwake kuhusu ulipaji wa madeni
ya maji kwa taasisi za serikali ,makampuni binafsi pamoja na wananchi.
“Kwenye huu ulipaji wa madeni ya maji kwakweli hizi taasisi
za serikali zimekuwa ni tatizo kubwa kwa upande wa madeni licha ya kuwa mamlaka bado inaendelea na
jitihada za kuhakikisha kuwa madeni hayo yanalipwa mapema”alisema.
Akizungumzia kwa upande wa shule za sekondari za serikali
Bi.Stanton alisema nazo zimekuwa zikisuasua
kwa kiasi Fulani kutokana na wao
kuweka kipaumbele mambo Fulani kwenye
shule zao.
Hata hivyo Ofisa Uhusiano huyo alisema kwa upande wa shule za sekondari za binafsi wao wamekuwa wepesi wa kulipa madeni
lakini kwa kufuatiliwa sana na
mamlaka ndipo wanalipa madeni hayo.
“Lakini pia licha ya kuwa
wanalipa lakini ni wajibu wao kutakiwa kulipa kwa wakati bila kufuatwa kwani kulipa ni wajibu wao
sababu wanatumia maji isitoshe kwa suala la shule ambalo ni muhimu zaidi”alisema.
Aidha
Bibi.Stanton alitoa wito kwa shule za serikali kuweka kipaumbele
ulipaji wa bili za maji kwani fedha hizo zinasaidia malipo ya
umeme,madawa kwenye maji ambayo yanatumia grama kubwa.
“Kwa ujumla grama za uendeshaji ni nyingi
hivyo ni vema shule na taasisi za serikali zikatambua umuhimu wa huo “alisema.
Hata hivyo Ofisa uhusiano huyo alipotakiwa kuzungumzia kiasi
kamili cha madeni ambayo mamlaka ya maji inadai alisema suala hilo lipo kwa
meneja ambaye ndiye ana takwimu sahihi.
0 comments:
Post a Comment