Habari na Ezekiel Kamanga,Mbozi.
Bwana
Paulo Sichone na wenzake 13 wote Wakazi wa Kijiji cha Myunga, Kata ya
Myunga, Wilaya ya Momba Mkoani Mbeya wamefutiwa mashtaka wamejikuta
wakibubujikwa na machozi ya furaha baada ya kuachiwa huru na mahakama ya
wilaya ya Mbozi mkoani hapo Oktoba 2 mwaka huu.
Watu
hao walikuwa wakikabiliwa na kesi namba 143/2012, wakituhumiwa kwa kosa
la kutumia silaha na unyang'anyi ambapo kwa pamoja wanadaiwa kuvunja
nyumba ya Bwana Benard Simundwe na kuiba mali zenye thamani ya shilingi
milioni 87, kinyume cha sheria ya makosa ya jinai kifungu cha 287(a).
"Kwa
pamoja mheshimiwa naiomba mahakama yako Tukufu kuwaachia huru
washtakiwa wote, kwa kutumia Kifungu cha 91 cha sheria na Jamhuri haina
nia ya kuendelea na kesi hiyo" alisema muendesha mashtaka mahakamani
hapo.
Baada
ya kauli hiyo ya mwendesha mashtaka, Wakili wa washtakiwa mheshimiwa
Edgar Bantulaki alikubaliana na mwendesha mashtaka, hivyo wateja wake
kuwa huru kuanzia Oktoba 25 mwaka huu tangu walipokamatwa Agosti 13
mwaka huu na wengi wao kudhalilishwa na Jeshi la Polisi wakati wa
operatioh hiyo.
Aidha
baada ya kesi hiyo kumalizika mahakamani washtakiwa hao walilakiwa na
ndugu zao wakiongezwa na Mwenyekiti wa kijiji hicho Bwana Satiel Japhet
Sikanyika na Diwani wa kata ya Iyunga Bwana mheshimiwa Godfrey Siame
ambao kwa pamoja wamesema wanamshukuru Mungu kwa shari lao kumalizika
kwani shughuli za uchumi zilizorota kijijini hapo kwani muda mwingi
walikuwa wakiutumia kuhudhuria kesi ya mahakamani na gharama kubwa za
nauli kutoka Myumba.
Kwa
upande wake nje ya mahakama wakili Edgar aliwataka wananchi hao
kutokuwa na risasi hivyo wasamehe na kupotezea kabisa hivyo wasamehe na
kusahau yote yaliyopita.
Pia
Mcungaji wa Kanisa la Moravian Tanazania, Jimbo la kusini Magharibi,
Mchungaji Isaya Simsokwe amewaambia wananchi wa Kijiji cha Myunga
kumtegemea Mungu wakati wao ndio maana ametetea na kuwashindia katika
kesi hiyo nzito ambayo imesababisha wengine kuuza Chakula ili
kukabiliana na keshi hiyo.
Katika
hali isiyokuwa ya kawaida mlalamikaji katika kesi hiyo Bwana Benard
Simunde, alionekana mahakamani hapo hali inayotia shaka utendaji wa
Jeshi la Polisi kwa kufadhili mtandao wa uhalifu, licha ya kukabiliwa na
kuhusika na vitendo vya mauaji lakini Polisi wamekuwa wakimwangalia
bila kuchukua hatua zozote na wakati meingine kunywa nae juice kama
ilivyokuwa imetokea Oktoba 25 Bwana Simundwe alipokuwa na askai katika
mgahawa uliopo Posta eneo la Kiwila Mbozi.
Hata
hivyo vielelezp vilivyowasilishwa kituo cha Tunduma na Mbozi vimetoweka
katika hali ya Tunduma na Mbozi vimetoweka katika hali ya kutatanisha
ilinayompa wakati mgumu Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mbeya Diwani
Athumani vilivyodhibiti vitendo vya rushwa vilivyokithiri katika vituo
mbalimbali .
0 comments:
Post a Comment