Pages


Home » » BAADA YA MAKABURI KUTELEKEZWA NA MAZINGIRA KUWA MSITU BOMBA FM REDIO YAONGOZA ZOEZI LA KUSAFISHA MKOANI MBEYA.

BAADA YA MAKABURI KUTELEKEZWA NA MAZINGIRA KUWA MSITU BOMBA FM REDIO YAONGOZA ZOEZI LA KUSAFISHA MKOANI MBEYA.

Kamanga na Matukio | 02:13 | 0 comments
 Baada ya mazingira ya makaburi ya Isanga kugeuka kuwa msitu na kuwa kimbilio wa la waharifu, vijana kuvuta bangi,kucheza kamali na ufuska, baadhi ya wananchi wamejitokeza kuanza kusafisha kufuatia Kampeni iliyofanywa na Kituo cha Redio cha Kurushia Matangazo cha Bomba FM 104.0MHz kilichopo Mkoani Mbeya baada ya Jiji kutelekeza bila kuyafanyia usafi kwa muda mrefu.
 Dada huyu hakubaki nyuma katika zoezi la kuokota karatasi na kuzichoma.
 Kaka huyu naye akijumuika katika zoezi la kukata miti.
 Mwandishi wa habari wa Kituo cha Redio cha Kurushia Matangazo cha Bomba FM 104.0MHz akiwajibika katika zoezi la usafishaji wa makaburi.
 Zoezi likiendelea.
 Baadhi ya wananchi waliojitokeza wakiendelea kukata vichaka.
 Akina mama hawakuwa nyuma na walifanya kazi kwa moyo mmoja.
 Mwanadada huu akiendelea kuchapa kazi ya kukikata kichaka.
Meneja Msaidizi ambaye pia ni Mwandishi wa habari wa Kituo cha Redio cha Kurushia Matangazo cha Bomba FM 104.0MHz na Mmiliki wa mtandao wa Kamanga na Matukio Blogu Bwana Ezekiel Kamanga, akihakiki majina ya wananchi waliohudhurika katika zoezi hilo.
 Mtuma salamu maarufu mkoani Mbeya almaarufu kwa jina la Mama Samweli akiendelea kuwajibika.
 Mkuu wa Kitengo cha Promotion,ambaye pia ni Mtangazaji na Dj wa Kituo cha Redio cha Kurushia Matangazo cha Bomba FM 104.0MHz na Mmiliki wa mtandao wa Chimbuko Letu Blogu, Ndugu Greyson Salufu Chatanda a.k.a Chris Bee akiwajibika katika ukataji wa vichaka.
 Mtangazaji wa Kituo cha Redio cha Kurushia Matangazo cha Bomba FM 104.0MHz Bi. Tunu Izack Lugombe akiendelea kuwajibika.
 Wadau wa salam na Mtangazaji wa Kituo cha Redio cha Kurushia Matangazo cha Bomba FM 104.0MHz Ndugu Shaban Nasorro a.k.a Sheby Leizer wakiendelea kusafisha eneo la makaburi hayo.
Sheby Leizer.(Picha zote na Ezekiel Kamanga)

NB:- Zoezi hili nzima litaendelea Ijumaa ijayo,shukrani kwa waliojitokeza kwa moyo mmoja na kwa Bomba FM redio kwa kampeni hii.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger