* Ni mchungaji wa Kanisa.
* Wawili wagunduliwa na Ujauzito
* Mmoja ashindwa kufanya mtihani.
Habari kamili na Ezekiel Kamanga,Mbozi.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi
Ipapa, Kata ya Ipunga, Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya Bwana Eliezeli
Nyalutogo Kyando,anatuhumiwa kuwapa mimba wanafunzi wawili wa darasa la
saba wa shule hiyo.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa
Bodi ya shule hiyo Bwana Amosi Silwimba, alipokuwa akitoa maelezo katika
Kituo cha Polisi cha wilaya hiyo, baada ya suala hilo kushindwa
kupatiwa ufumbuzi katika kikao cha Bodi ya shule hiyo hivi karibuni.
Imedaiwa katika kikao hicho mwalimu
huyo kwa nyakati tofauti aliwapa mimba wanafunzi hao, ambapo mmoja
alikuwa na mimba ya miezi sita na mwingine miezi mitatu hivyo kupelekea
binti mmoja kushindwa kufanya mtihani wa Taifa uliofanyika mwezi
Septemba mwaka huu(Majina yamehifadhiwa).
Aidha Mwalimu Mkuu Kyando,amedaiwa
kuwa ni Mchungaji mwandamizi wa kanisa moja la Kipentekoste (jina
linahifadhiwa) lililopo Kata ya Ihanda wilayani humo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya
shule hiyo na viongozi wenzake walipata malalamiko kutoka kwa wazazi wa
wanafunzi hao baada ya kuonesha mabadiliko ya kimaumbile na walipo
wadadisi walidai kuwa mwalimu huyo ndio mhusika, na mmoja alidai kuwa
alikuwa akimpikia chakula nyumbani kwake na kutendewa ukatili huo kwa
kushirikiana kimapenzi kwa awamu tatu na kumpa ujauzito ambao una miezi
sita.
Kwa uapnde wake Afisa Elimu wa Shule
za msingi wilayani humo amesema kuwa suala hilo lipo juu ya uwezo wake
hivyo mwenye kutolea majibu ni Mwajiri ambaye ni Mkurugenzi wa Wilaya.
Hata hivyo Mkurugenzi wa Wilaya hiyo
Bwana Levison Chilewa, amesema kuwa taarifa hizo bado hazijamfikia na
kwamba yupo nje ya Ofisi na kuahidi kulifuatilia.
0 comments:
Post a Comment