Na Ester Macha
Serikali
ya Tanzania ilitangaza sera ya Kilimo Kwanza kama njia maalumu ya
kitaifa ya kuongeza kasi ya kuleta mapinduzi ya kilimo nchini na kuinua
pato la wakulima Kwanza inajumuisha mikakati inayolenga katika kutatua
changamoto mbalimbali zinazokabili kilimo chetu na kutumia fursa lukuki
tulizonazo kujiondolea umaskini wa kipato.
Azima
ya Kilimo Kwanza ilibuniwa chini ya Baraza la Taifa la Biashara (TNBC)
ambalo ni mfumo wa mashauriano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndiye mwenyekiti wa Baraza hilo.
Licha
ya nchi yetu kuwa na hekta milioni 44 za ardhi inayofaa kwa kilimo, ni
asilimia 23 tu ndiyo inayotumika. Kuna hekta milioni 29 zinazofaa kwa
kilimo cha umwagiliaji na maji ya kutosha yapo lakini ni asilimia moja
tu iliyo chini ya umwagiliaji.
Aidha,
licha ya Tanzania kuwa na maziwa na mito yenye maji ya eneo la kilomita
za mraba 62,000, ukanda wa pwani ya Bahari ya Hindi wenye urefu wa
kilomita 1,424 na kilomita za mraba 223,000 za ukanda maalumu wa
kiuchumi baharini (Exclusive Economic Zone), lakini maji hayo mchango
wake kwa pato la taifa na la mtu mmoja mmoja bado ni hafifu .
Moja ya changamoto ambazo zimekuwa
zikiwakumba wanawake waliopo vijijini ni ugumu wa maisha uliopo na
hivyo kulazimika kujikita zaidi katika kilimo ili waweze kuondokana na
hali duni ya kimaisha iliyopo miongoni mwao.
Ili
kuhakikisha kuwa wanaondokana hali ngumu ya kimaisha wanawake waliopo
vijijini wamekuwa nguzo kuu ya kilimo kuliko wanaume kutokana na na wao
kuwa walezi wa familia katika nyumba zao.
Hivi
karibuni mwandishi wa makala haya alitembelea katika kata ya Ijombe
wilaya ya Mbeya
mjini kuona hali halisi ya maisha ya wanawake hususani suala la kilimo
ambapo ilionekana kuwa wanawake na watoto wanaendelea kunyanyasika
kutokana na badhi ya wanaume kutumia mwanya huo kusafirisha mazao
mijini na fedha ambazo zinapatikana
baada ya kuuza mazao hutumia kwa anasa Ili kila mwananchi aweze kuishi vizuri na familia hakuna budi mazao yanayolimwa.
Wakizungumza wanahabari wanaharakati wa mtandao wa kijinsia
Tanzania (TGNP) kijijini hapo leo baadhi ya wanawake wa kata hiyo ya Ijombe
wamesema kuwa kukosekana kwa masoko katika kata hiyo ndiko kunapelekea wao na
watoto kuendelea kunyanyasika katika mgawanyo wa kipato kinachotokana na mavuna
wanayoyapata .
Zuwena Mwakyoma na Atuganile Mwasanga wakazi wa kata hiyo ya
Ijombe wamesema kuwa pamoja na kuwa wakati wa kuandaa mashamba
kwa kulima na kutunza mazao hayo hadi yanafikia wakati wa kuvunwa ila ikifika
wakati wa mavuno wanaonyanyasika zaidi ni wanawake na watoto huku wanaume wao
wakitumia nafasi hiyo kujineemesha mijini .
Zuwena anasema kuwa wakati kata hiyo ya Ijombe ikiwa ni moja
kati kata zinazoongoza kwa kuzalisha mazao mbali mbali ya kibiashara ila bado
serikali haijaweza kuwakomboa wakulima hao kwa kujenga soko la mazao ambalo
litawasaidia wakulima wa kata hiyo kuuza mazao yao na kunufaika na kilimo .
“Leo tumekuwa tukishuhudia jinsi ambavyo sisi wanawake na
watoto tunavyonyanyasika na kilimo na kushuhudia baadhi ya wanawake
wakinyanyasika kwa waume zao kuongeza wanawake wakati wa mavuno kutokana na wao
kuwa wasimamizi wakuu wa mazao hayo ….wamekuwa wakiyasafirisha kwa usafiri wa
mikokoteni hadi mjini na huku wakiuza pesa zote wanatumika katika pombe na
kuhonga wanawake”.
Hivyo anasema njia pekee ya wanamke na mtoto wa pembezoni
mwa miji kuweza kukombolewa ni serikali kuweka utaratibu wa kujenga masoko
katika kata hiyo na kata nyingine ambazo zipo pembezoni na miji .
Huku Atuganile akidai kuwa mbali ya baadhi ya wanaume wa
kata hiyo kuendelea kuwanyanyasa wakati wa mavuno kwa kuwaongezea wanawake ama
wapenzi katika nyumba zao ila bado hata madalali wamekuwa ni kikwazo kikubwa
kwani wamekuwa wakifika na kununua mazao yakiwa mashambani .
Anasema kuwa madalali hao wamekuwa wakifika kununua mazao
katika mashamba hayo hata kabla ya kuvunwa na sehemu kubwa ya wanaoathirika na
mfumo huo wa madalali ni wanawake wajane ambao hawana uwezo wa kutafuta masoko
wala kupata fedha za kusafirishia mazao hao na hivyo kukubali kuuza mazao yao
kwa bei yeyote ile .
“Kuna baadhi ya kaya ambazo zinaongozwa na mama na baba
mwenye moyo wa upendo katika familia yake zimekuwa zikinufaika na kilimo
kutokana na kuuza mazao kwa ushirikiano na pesa hutumika kwa matumizi mazuri
ila baadhi ya kaya suala la masoko ni kilimo endelevu”.
Pia anasema suala la ushuru limeendelea kuwa kero kutokana
na serikali ya wilaya kuwatoza ushuru mara mbili mazao yakiwa shambani na pindi
yanapopelekwa sokoni Uyole .
Deus Mwambaje mkazi wa kijiji cha Iwalanje kata hiyo ya
Ijombe akijibu madai ya wanawake hao alisema kuwa si wanaume wote ambao
wamekuwa wakinyanyasa wake zao wakati wa mazao na kuwa badhi ya kaya zimekuwa
na ushirikiano kwa kulima pamoja na kuuza kwa utaratibu mzuri ila badhi ya kaya
zimekuwa zikiongoza kwa migogoro na kesi wakati wa mavuno kutokana na
wasimamizi wa familia hiyo ambao ni wanaume kuwa na mfumo dume kwa kuuza mazao
na pesa kuhonga wanawake mjini.
"Hili
ni tatizo kubwa kwa baadhi ya familia kwani inaonyesha ni jinsi gani
wanaume ambavyo wamekuwa wanyanyasi wakubwa katika familia zao huku
wakisahau kuwa walezi wakuu wa wa familia ni wanawake ni muhimu wanawake
nao wakapewa kipaumbele"anasema mwanaume.
Anasema
kuwa pamoja na kwamba yeye ni mwanaume lakini vitendo ambavyo vimekuwa
vikitokea katika vimekuwa ni vikwazo kwake na kuonyesha kuwa wanawake ni
watu wa kuonewa kila wakati,mazao yanalimwa kwa ushirikiano kwa pamoja
lakini unashangaa unakuta kipindi cha mavuno ugomvi unakuwa mwingi ndani
ya familia.
Mkazi
mwingine Bi. Yusta Mwambula anasema kuwa suala la kunyanyaswa kutokana
na mazao kwa wanawake wa eneo hilo ni kitu cha kawaida ,kwani hata
familia zilizo nyingi zina migogoro mingi kwani ikifika kipindi cha
mavuno mwanaume anavuna mazao na kuuza na kuondoka zake hivyo kwa
ujumla hali ni mbaya.
Hata hivyo alidai kuwa pamoja na kuwa kata hiyo inaongoza
kwa kulima nyanya, njegere ,viazi ,karoti na vitunguu pamoja na mazao mengine
ya biashara ila hakuna soko hata moja.
Afisa biashara wa wilaya ya Mbeya Castro Temihanga
alithibitisha madai ya wanawake hao wa kata ya Ijombe kuwa ni kweli kata hiyo
mbali ya kuongoza kwa uzalishaji ila hakuna soko na kuwa jitihada za
Halmashauri kuzungumza na watu wa SIDO ili kusaidia kujenga soko eneo hilo
zinafanyika.
0 comments:
Post a Comment