*Yaongeza ajira kwa Watanzania,iko mbioni kujenga Chuo cha Wauguzi.
Habari na Ezekiel Kamanga, Rungwe.
Hospitali
ya Mission ya Igogwe iliyopo Kata ya Kinyala, Wilaya ya Rungwe Mkoani
Mbeya imeadhimisha jubilee ya miaka 50 tangu kuanza kutoa huduma ya
matibabu mwaka 1962 na sherehe hizo kufikia kilele chake Oktoba 18 mwaka
huu.
Hafla
hiyo iliongozwa na Baba Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo kuu la Mbeya
Evaristo Chengula, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya
Ndugu Abbas Kandoro ambaye katika sherehe hiyo aliwakilishwa na Mkuu wa
Wilaya Rungwe ndugu Crispin Meela.
Katika
hotuba yake Baba Askofu ameiomba Serikali kufanya haraka kutoa eneo la
ardhi ili hospitali hiyo iweze kupanua shughuli zake ikiwa ni pamoja
kuanzisha Chuo cha Wauguzi ili kuisaidia Serikali katika uboreshaji wa
sekta ya Afya nchini.
Askofu
Chengula amesema Kanisa la Kikatoliki lina nia ya kuleta maendeleo
zaidi katika hospitali hiyo licha ya wananchi 9 kugoma kuachia maeneo
yao ili kupisha ujenzi wa majengo ya hospitali kwa ajili ya chuo na
mahabara ya kisasa.
Aidha
uongozi wa hospitali hiyo ulimweleza mgeni rasmi kuwa zaidi ya watu
150,000 hupatiwa huduma ya malazi kwa mwezi na kwamba zaidi ya wagonjwa
400,000 hutibiwa na kurejea makwao.
Vilevile
hospitali hiyo imelenga kutoa ajira kwa watumishi 120 wa kada
mbalimbali wakiwemo madaktari, wauguzi, mafamasia na kada nyingine na
kwamba kila mmoja waweze kuifikisha hospitali hiyo ambapo kwa mwaka
imeweza kuhudumia zaidi ya wagonjwa 5600 na huduma ya upasuaji kwa
wagonjwa zaidi ya 503.
Hata
hivyo hospitali hiyo inakabiliwa na upungufu wa wafanyakazi wa kada
mbalimbali na uongozi umeitaka Serikali kuongeza watumishi, kwani
hospitali hiyo imekuwa ikitoza kiasi kidogo cha fedha, hali iliyopelekea
kuwa kimbilio kwa wananchi wengi kutoka mikoa ya Rukwa, Iringa na
Ruvuma pia nchi za Zambia na Malawi kutokana na ubora wa huduma
unaotolewa na hospitali hito.
Wakati
huohuo hospitali inakabiliwa na changamoto za upungufu wa vitanda,
ambapo hivi sasa kuna vitanda 140 za kulaza wagonjwa katika wadi tano
zilizopo, ukosefu wa gari la kubebea wagonjwa, ulipaji wa mishahara kwa
wakati, pesa za kulea watoto wanaokaa katika mazingira hatarishi na
hawajiwezi, ukatikanaji wa umeme na barabara mbovu ambayo huweka adha
kwa wagonjwa pindi wanapokimbizwa katika hospitali hiyo.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro ambaye aliwakilishwa na
Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Bwana Crispin Meela amesema ombi la ardhi
litaanza kufanyiwa kazi Oktoba 22 mwaka huu na suala la barabara
atawasiliana na wakala wa barabara nchini(TANROADs), ili baada ya hiyo
iingia katika mpango wa mkoa ili kuboresha miundombinu katika hospitali
hiyo na kwamba barabara hiyo yenye urefu wa Kilimita 4 iwe lami.
Askofu
Chengula amewashukuru wafadhili waliolazwa katika Hospitali hiyo na pia
anaomba ruzuku ya madawa katika bohari ya serikali(MSD) huku huduma za
watu wanaoishi na VVU, pia huduma ya mama na mtoto ambayo ilipaswa
kutolewa na serikali.
Mbali
na sherehe ya Jubilee Askofu Chengula alizindua mnara rasmi wa Jubilee
hiyo na kuwapa daraja la kipaimara vijana na wazee wapatao 200 katika
sherehe iliyofana na kuwataka waeende katika maadili yatakayompendeza
Mungu na wanadamu pia nao kuleta amani na upendo kwa waumini na
wasiokuwa waumini kwani kumekuwa na matukio ya uhalifu ambao wengi
hufanya na watu waliopata kipaimara hivyo vijana wasifurahie tendo hilo
tu bali wafuate Mema kwa kristo.
0 comments:
Post a Comment