Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Kitendawili
cha hatima ya kesi namba 143/2012 kimeshindwa kuteguliwa na Hakimu wa
Mahakama ya wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya baada ya kesi hiyo kuahirishwa
hadi Oktoba 25 mwaka huu baada ya Oktoba 18,mahakama hiyo kushindwa
kutoa maamuzi kama ilivyoahidi Oktoba 15 mwaka huu.
Kesi
hiyo inayomhusu Bwana Paulo Sichone na wenzake 12 ilikuwa itolewe
maamuzi Oktoba 18 mwaka huu lakini jalada la kesi hiyo kudaiwa kuwa
halipo mahakamani kwa mujibu wa maelezo ya Mwendesha Mashtaka.
Oktoba
18 mwaka huu, Mwendesha Mashtaka ameiambia mahakama hiyo kuwa jalada
hilo limepelekwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali mkoani hapa, hali
iliyopelekea washtakiwa kuendelea kusota mahabusu baada ya mwendesha
mashtaka kukataa dhamana.
Hata
hivyo katika hali isiyokuwa ya kawaida Jeshi la Polisi limemwachia kwa
dhamana Bwana Benard Simundwe, anayedaiwa kujihusisha na mtandao wa
majambazi licha ya vielelezo kuwasilishwa Polisi Kituo cha Tunduma na
Mbozi na Polisi kudai kuwa havipo hali iliyozua maswali mengi kwa
wapenda haki na amani tukio lilitohusishwa na kuwepo kwa Rushwa ndani
yake na kuthibitisha kuwa mwenye pesa siyo mwenzako kutokana na wanyonge
kusota mahabudu huku wenye pesa wakitanua mitaani.
0 comments:
Post a Comment