Pages


Home » » KUFUATIA WIZI WA MITA ZA MAJI KUKITHIRI MKOANI MBEYA MAMLAKA YA MAJI YAWATAKA WANANCHI KUTOA USHIRIKIANO

KUFUATIA WIZI WA MITA ZA MAJI KUKITHIRI MKOANI MBEYA MAMLAKA YA MAJI YAWATAKA WANANCHI KUTOA USHIRIKIANO

Kamanga na Matukio | 02:49 | 0 comments
Na Esther Macha, Mbeya
KUFUATIA wizi wa mita za maji kukifiri Mkoani Mbeya Mamlaka ya maji imesema kutokana na kutambua umuhimu wa huduma hiyo wananchi wametakiwa kutoa ushirikiano kwa mamlaka hiyo kwa mtu yeyote ambaye anajihusisha na wizi wa mita hizo ambazo zimekuwa zikiingizia hasara mamlaka.

Akizungumza na majira ofisini kwake jana Ofisa Uhusiano wa Mamlaka hiyo Bibi.Neema Stanton alisema  tatizo hilo  ni kubwa kwa mamlaka la wizi wa wizi ambalo si zuri na linakwamisha utendaji wa kazi wa kila siku.

“Maeneo yote ya Jijini mbeya tunaomba wananchi watoe ushirikiano wa dhati wa kuhakikisha  suala hili la wizi wa mita linakwisha hivyo wananchi watumie namba hii kutoa taarifa ambayo ni 0800755533 ili kuweza kuwabaini watu hawa”alisema.

Akizungumzia kuhusu maeneo ambayo yanaibwa mita alisema  ni Kata ya Ilemi,Iganzo,Isanga  hizi kwa ujumla ndo zimekuwa na matatizo ya kuibwa mita  mara kwa mara  katika maeneo yao.

Bibi.Stanton alisema  kuhusu wizi wanaendelea na uchunguzi  kujua mita hizo baada ya kuibwa zinafanyiwa nini  na kuwafahamu wahusika wakuu ili waweze kuchukuliwa hatua haraka kutoklana na wizi huo.

Hata hivyo alitaja idadi ya mita zilizoibwa kuwa ni  zaidi ya 300  ambazo zimelipotiwa  kiofisi  na kuongeza kuwa hasara ambayo wanaipata mara baada ya mita hizo kuibwa ni upotevu wa maji ambayo hutiririka muda wote  kutokana na kuwa wazi.

Akizungumzia  hasara ambayo mamlaka inapata alisema baada ya mita hizo kupotea alisema  ni kununua mita zingine licha ya kuwa wateja huchangia kiasi Fulani bado inaleta hasara kwa  mamlaka.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger