Home »
» WATAKA SUMATRA,POLISI KUKAGUA MABASI MABOVU
WATAKA SUMATRA,POLISI KUKAGUA MABASI MABOVU
Hawa Mathias,Mbeya.
BAADHI
ya wananchi wanaotumia vyombo vya usafiri maarufu (daladala) Mkoani
Mbeya wameomba mamlaka ya usafirishaji wa nchi kavu na majini
(SUMATRA) kushirikiana na jeshi la polisi kufanya ukaguzi wa
haraka wa magari mabovu ili kuweza kuthibiti ajari za barabarani
zinazochangiwa na ubovu wa vyombo vya usafiri.
Wakizungumza
na Mwananchi baadhi ya wananchi wanaosafiri kati Sokomatola kwenda
uyole na sokomatola Mbarizi wamesema kuwa vyombo vingi vya usafiri
havina sifa ya
kusafirisha abiria na badala yake wamiliki wamekuwa wakitanguliza
maslai ya fedha badala ya uhai wa abiria na mali zao.
"Ifikie
wakati idara husika kusimamia hilo na kusikiliza kero za wananchi na na
kuwataka
askari wa jeshi la polisi kitengo cha usalma barabarani kutojenga
mazoea na madereva na makondakta na badala yake wafanye kazi kwa
kuzingatia maadili na kanuni za kisdheria ili kukabiliana na hali hiyo
ili kuthibi hali ya usalama barabarani "Alisema Jordan Mwaisanila mkazi
wa uyole
"Tunaomba sumatra kushirikiana na jeshi la polisi
na umoja wa chama cha madereva ili kuweza kukaa pamoja na kujua nini cha
kufanya ili kuthibiti hali hii kwani mabasi mengi ni mabovu na madereva
wengi wamekuwa wakikiuka sheria za usalama barabarani kwa kuendesha
magari kwa mwendo kasi,kutovaa sare na kutoa lugha chafu kwa
abiria"Walisema.
Naye Mkazi wa Mji mdogo wa mbarizi Selina
Jonhson alisema kuwa sasa ifikie wakati jeshi la polisi kitengo cha
usalama barabani kuweka mikakati kabambe ili kuhakikisha linaendesha
zoezi kwa kuzingatia kanuni na sheria na kutomuonea kwa kutoza faini
kubwa ili kuweza kutoa fundisho kwa
wamiliki wa vyombo vya usafiri waweze kutambua wajibu wao wa kuvifanyia
matengenezo vyombo vya usafiri na si kutanguliza masli ya fedha mbele.
"Sasa
ifikie wakati hata polisi wa usalama barabarani akufanya ukaguzi wa
magari na kufanya mazoea na madereva na makondakta na hivyo ni jukumu
lenu kutambua nini kinachowaweka barabarani kwani kukagua leseni na
mataili bado hamjatambua ubovu wa vyombo vya usafiri"Alisema Jordan
Mwasakyeni.
Johnson alisema kuwa wamiliki wa vyombo vya
usalama wanapaswa kutambua majukumu yao kwa watazania kwa kufanya
ukarabati na matengenezo ili kuepuka hasara na vifo vya wananchi
vinavyotokana na ajari za barabarani.
0 comments:
Post a Comment