Mwandishi wa Habari wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1) Ndugu Hosea Cheyo.
Habari na Ezekiel Kamanga, Iringa.
Mwandishi wa habari wa wa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC1
mkoani Mbeya Bwana Hosea Cheyo ameibiwa Kamera na kompyuta pakato yaani
Laptop vyenye thamani ya shilingi 1,800,000 katika nyumba ya kulala
wageni iitwayo Happy Lodge iliyopo jirani na kituo kikuu cha mabasi cha
Iringa, Oktoba 2 mwaka huu majira ya 1:30 asubuhi.
Mwandishi
wa habari huyo alikuwa mkoani Iringa kuhudhuria semina ya waandishi wa
habri wa Nyanda za Juu Kusini inayohusu mchakato wa Katiba iliyoandaliwa
na Baraza la Habari nchini MCT kuanzia Oktoba 22 mwaka huu hadi Oktoba
24 mwaka huu katika Ukumbi wa Maktaba uliopo Manispaa ya Iringa.
Bwana
Cheyo amesema Oktoba 24 asubuhi alipokuwa kuoga alifunga mlango kwa
ufunguo na aliporudi alishangaa kuona vifaa vyake havipo, hali
iliyomfanya kutoa taarifa kwa mhudumu wa nyumba hito ya kulala wageni na
hakuwa na maelezo ya kutosha.
Mwandishi
huyo amedai kuwa mbinu iliyotumika kufungua mlango wake ni kutumia
ufunguo bandia na kisha wezi hao kuingia kiurahisichumbani humo na
kuondoka na vifaa vyake vya kazi.
Aidha
Bwana Cheyoaliotoa taarifa Kituo cha Polisi Mkoani humo na kufunguliwa
jalada lenye namba IR/RB/6350/012 na kwamba Jeshi la polisi
linamshikilia mhudumu wa nyumba hiyo ya kulala wageni kwa mahojiano
zaidi.
Hata
hivyo ilibidi Bwana Cheyo kushindwa kuendelea na semina ili
kushughulikia tatizo hilo, huku Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa
Habari mkoani Mbeya Bwana Christopher Nyenyembe, amempa pole mwandishi
huyo wa TBC kwa kuibiwa nyaraka muhimu na kuwataka wamiliki wa nyumba za
wageni kukomesha vitendo vya wizi vinavyofanywa na wahudumu wao.
0 comments:
Post a Comment