Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
*Mwananchi mmoja achomwa mkuki,Polisi wakimbia.
Ugomvi
baina ya Wafugaji wa Wakulima umezuka katika Kijiji cha Simike -
Utengule Usangu, Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya na kusababisha mwananchi
mmoja anayefahamika kwa jina Abeli Mwakyoma kujeruhiwa baada ya
kuchomwa mkuki na kundi la wafugaji wa jamii ya Kisukuma.
Wananchi
watatu wanaofahamika kwa jina la Bi. Magreth Simwela, John Kayange na
Richard Mwasyanga walinusurika kupigwa na kundi la wafugaji waliokuwa na
kundi la ng'ombe, hali iliyopelekea kutoa taarifa katika Kituo cha
Polisi cha Igurusi.
Aidha
Polisi wa kituo hicho walifanikiwa kuwakamata Juma Mwambeta, Daniel
Edward, Stephen, Walusungo Vaisi na Vedasto Simwaba wakidaiwa
kuwafungulia ng'ombe kutoka zizini
na mara baada ya kupata taarifa, Polisi walilazimika kwenda eneo la
tukio na kukuta kundi jingile la ng'ombe likila mazao shambani.
Baada
ya ng'ombe kukusanywa mifugo hiyo kundi la wafugaji lilianza
kuwashambulia Askari na wakulima kwa kutumia silaha za fimbo na mikuki,
hali iliyopelekea Polisi hao kukimbia..
Kupitia
sakata hilo wafugaji walifanikiwa kumkamata Bwana Abeli Mwakyoma na
kuanza kumshambulia na alipofanikiwa kukimbia alichomwa mkuki kiunoni na
baada ya umbali kadhaa aliomba msaada wa kunasuliwa mkuki huo na
kukimbizwa katika Hispitali ya Chimala Mission,ambapo alilazwa na
kuruhusiwa Oktoba 9 mwaka huu baada ya kupatiwa huduma ya matibabu.
0 comments:
Post a Comment