Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Mwanamke
mmoja aliyefahamika kwa jina la Mary Jimmy (55 - 60), Mkazi wa Barabara
ya Tatu, Sokomatola Jijini Mbeya amefariki dunia alipokuwa aliabudu
katika Ibada ya asubuhi(Morning Glory) kwenye Kanisa moja kubwa eneo la
Kabwe jijini hapa Oktoba 23 mwaka huu.
Tukio
hilo lilimetokea majira ya saa 1:30 asubuhi ambapo imedaiwa kuwa
marehemu alifika kanisani hapo majira ya saa 12:30 kwa nia ya kufanya
ibada ndipo akiwa katika maombi alianguka chini na waumini walifanya
maombi bila mafanikio mpaka walipoamua kumpeleka katika Hospitali ya
Rufaa na kuthibitisha kifo chake.
Mdogo
wa marehemu ambaye hakupenda kutajwa jina lake kwa madai kuwa si
msemaji wa familia alisema kuwa marehemu aliondoka nyumbani akiwa mzima
kabisa hivyo kifo hicho kimemshitua mno.
Mwili
wa marehemu unafanyiwa uchunguzi katika Hospitali ya Rufaa na mazishi
yanataraji kufanyika leo katika makaburi ya Nonde jijini hapa. Marehemu
ameacha mtoto mmoja wa kiume.
Tukio
jingine Mkazi mmoja wa Iziwa, Jijini hapa Mbwiga Mwalungwe(60),
amefariki dunia baada ya kujinyonga nyumbani kwake kwa kutumia waya wa
simu Oktoba 24 mwaka huu baada ya marehemu kumpiga mkewe.
Inadaiwa
marehemu alimpiga mkewe aitwaye Bi. Taines Mbwiga(45) Oktoba 23 hali
iliyompelekea kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa Jijini hapa ambapo
alipewa PF3 kwa ajili ya kutibiwa na kulazimu kulazwa hospitalini hapo.
Baada
ya mkewe kulazwa hospitalini, Jeshi la Polisi lilianza kufuatilia tukio
hilo ndipo marehemu alipogundua kuwa anakabiliwa na mkono wa sheria
aliamua kuchukua uamuzi mgumu kwa kuchukua waya wa simu majira ya saa 4
kamili asubuhi Oktoba 24, kisha kujinyonga nyumbani kwake.
Aidha
polisi walifika eneo la tukio majira ya saa 6:00 mchana na kuuchukua
mwili wa marehemu hadi hospitali ya rufaa kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Hata
hivyo hali ya Bi, Taines inaendelea vema ambapo ameruhusiwa kutoka
hospitalini Oktoba 2 na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali
hiyo.
Kwa
upande wake Balozi wa mtaa huo Bwana Chaina Juma amethibitisha kutokea
kwa tukio hilo na kwamba anawaachia jeshi la polisi kufanya uchunguzi
ili kupata kiini hasa cha Bwana Mwalungwe kujiua kwa kujinyonga.
0 comments:
Post a Comment