* Marehemu adaiwa kufariki baada ya kula nyama ya tambiko.
* Mwingine akumbwa na wazimu baada ya kukata mti.
********
Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Watu
wanne wakazi wa Kijiji cha Wimba Mahango, Kata ya Ruiwa, Wilaya ya
Mbarali Mkoani Mbeya wamenusurika kifo baada ya wananchi wenye hasira
kali kutaka kuwazika wakiwa hai, baada ya kudaiwa kutaka kumuua Wiston
Nsanja(52), kiushirikina baada ya marehemu kudaiwa kula kwa pupa nyama
ya tambiko mapema mwezi Julai mwaka huu.
Watu
hao wamefahamika kwa majina ya Julius Sibela, Julius Nsalanga(Bundala),
Rajab Benyanga(Putu) na Jailos Mdanga(Kazi), ambao wote wanadaiwa
kumloga kishirikina marehemu baada ya kukiri mbele ya wakazi wa kijiji
hicho kabla ya kifo chake na ndipo alianza kuugua mwezi Julai na
kutibiwa katika Hospitali mbalimbali bila mafanikio hadi kifo
kilipomchukua Oktoba 5 mwaka huu majira ya saa tatu usiku.
Aidha
kabla ya kifo cha Wiston wananchi hao wakiwa na hasira walianza
kumshaka mtuhumiwa mmoja baada ya mwingine na kufanikiwa kuwakamata
wawiliambao ni mzee Benyanga na Sibela na kabla ya kuchukuliwa hatua
zozote, Afisa Mtendaji wa kijiji Bwana Naftali Sengele alipewa taarifa
na wasamaria wema na yeye kutoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Kijiji Bwana
Wiston Kazimoto.
Kufuatia
taarifa hizo viongozi hao hawakusita kutoa taarifa Ofisi ya Kata ya
Ruiwa na Kaimu Afisa Mtendaji wa Kata Bwana Zephania Mgaya, kwa
kushirikiana na Mugambo wa kijiji walifanikiwa kuwanasua mikononi mwa
wananchi wazee hao na kuwasalimisha katika Ofisi ya kata na baadae
kuwapeleka Polisi katuo cha Rujewa kwa usalama zaidi huku wazee wengine
Nsalanga na Mdanga wakitokomea kusikojulikana.
Mnamo
majira ya asubuhi ya Oktoba 6 mwaka huu, wananchi waligoma kumzika
marehemu wakidai azikwe na waliosababisha kifo chake yaani waze wanne
ambao ni Mzee Nsalanga, Benyanga, Sibela na Mdanga kauli ambayo waliitoa
katika Mkutano wa hadhara nyumbani kwa marehem, pia ilidaiwa wazee hao
ndiyo waliosababisha mwanamke mmoja kukumbwa na ugonjwa wa wazimu baada
ya kukata mti unaodaiwa kutumika katika matambiko.
Hata
hivyo wananchi walikubali kumzika marehemu baada ya Afisa mtendaji
kuwakamata watuhumiwa na kuwapeleka polisi na wananchi kudai hawatakiwi
teba kijijini hapo.
0 comments:
Post a Comment