Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya Diwani Athumani,akizungumza suala
la kukamatwa kwa viongozi wa Chama cha walimu pamoja na walimu
wamekamatwa kutokana na tuhuma za kuhamasisha wezao kugoma jambo ambalo
ni kinyume cha sheria katika Mji mdogo wa Tunduma Mkoani Mbeya.
*******
Habari na Ezekiel Kamanga, Tunduma.
Watu
9 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya,wakiwemo viongozi wa
Chama cha walimu na walimu wenyewe kufuatia vurugu zilizosababisha
hasara zaidi ya shilingi milioni 100 wakati wa mgomo wa walimu ulioanza
juzi.
Kitendo
cha walimu hao kugoma kuingia madarasani kufundisha kwa kushirikiana na
wanafunzi walifanya maandamano ya amani ya kudai haki ya masilahi
ikiwemo mishahara na tukio linadaiwa kutumiwa vibaya na wahalifu kwani
walitumia nafasi hiyo kufanya uhalifu kwa kuiba mali za watu.
Wahalifu
hao walichoma ofisi za Halmashauri ya Mbozi ndani ya Mji mdogo wa
Tunduma na kuiba mali zilizokuwemo kama kompyuta 5 za ofisi, pikipiki
yenye namba STK 6264, kumbukumbu na nyaraka mbalimbali.
Wahalifu
hao walivunja milango ya ofisi zote, kuvunja vioo vya magari ya
kubebea taka aina FAW SM 8726, na kuiba betri mbili za gari hilo na
gari dogo aina ya Nissan lenye namba SM 2858 mali ya mamlaka hiyo.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani , aliwataja
watuhumiwa hao wanaodaiwa kuhusika na uhalifu na kusababisha hasara ya
shilingi milioni 117, 515,000 kuwa ni Mexon Mbilinyi(27) mkazi wa
Mtaa wa Maporomoko, Akida Kondo(25) mkazi wa Mtaa wa Chapwa, Chalres
Rupia(29) mkazi wa Mwaka,Athumani Mgala(39) mkazi wa migombani.
Wengine
ni Stela Garbert(20) mkazi wa Mtaa wa Migombani,Atiliyo Benard(28)
mkazi wa Mkurungu nchini Zambia, Nikodemus Exavely(17), Mashaka
Amoni(17) wote ni wakazi wa Mtaa wa Kaloleni - Tunduma na James
Kabuje(29) mkazi wa Mtaa wa Mabatini - Tunduma.
Diwani,
alisema kuwa watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kuhusika na uhalibifu
wa ofisi ya halmashauri ya mji mdogo wa tunduma ikiwa na kuiba mali
yenye thamani zaidi ya milioni 100 na kwamba wote kwa pamoja
wamefikishwa mahakamani leo.
Akizungumzia
suala la kukamatwa kwa viongozi wa Chama cha walimu pamoja na walimu
alisema watuhumiwa hao wamekamatwa kutokana na tuhuma za kuhamasisha
wezao kugoma jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Aliwataja
wahusika hao kuwa ni Mwalimu wa Patro Mangula na ni Katibu wa chama cha
walimu wilaya ya Kyela ambapo inadaiwa kuwa kiongozi huyo alikuwa
akishirikiana na watu wengine kupita mashuleni kuhamasisha walimu
waliokuwa wanaendelea na kazi ya kufundisha wajiunge na mgomo.
Wengine
ni Mwalimu Emanuel Kyejo wa shule ya msingi Mbebe Wilaya ya Ileje na
mjumbe wa chama cha walimu wilaya ya Ileje, Anyakingwe Lwinga na mjumbe
wa chama cha walimu ambapo wote kwa pamoja wanatuhumiwa kuhamasisha
walimu kugoma.
Aidha,
katika uhalifu wa Tunduma, Kamanada Diwani alisema kuwa polisi Mkoani
Mbeya kwa kushirikiana na wananchi walifanikiwa kuokoa Mabati 168,
Printa moja na mita mbili za maji, Bendera moja ya Taifa na photocopy
mashine.
Pia,
Kamanda Diwani alitumia nafasi hiyo kutoa ufafanuzi kwa nini askari
wake walitumia Bomu na risasi katika vurugu hizo ambapo alisema kuwa
Bomu hilo lilitumiwa kulitawanyisha kundi kubwa la watu lililokuwa
linazidi kuelekea kwenye ofisi za serikali pamoja na Taasisi za kibenki
na kwamba hakuna madhara yaliyojitokeza.
“Baadhi
ya watu wamekuwa wakiipotosha jamii kuwa askari walitumia bomu
kuwatawanya wanafunzi na ndio sababu za wananchi kuanzisha vurugu jambo
hilo si kweli kwani bomu lilitumiwa baada ya kundi la wahuni lililokuwa
likivamia ofisi na kuiba mali zilizomo ndani,”alisema.
Alisema,
wakati kundi hilo linafanya vurugu tayari wanafunzi walikuwa wamerejea
kwenye makao yao lakini kundi hilo la wahuni ndio lilikuwa likizidi
kujikusanya na kuendelea kufanya uhalifu huo huku baadhi wakiwa
wanaelekea kwenye eneo la Benki.
“Baada
ya walinzi wa Benki kuona kundi hilo linaikaribia benki askari walipiga
risasi mbili juu ili kuwatawanya na kwamba zoezi hilo lilisaidia
kuwarudisha watu hao waliokuwa na lengo la kufanya uhalifu katika benki
hiyo ,”alisema
Aidha,
Diwani aliitaka jamii kuondoa mawazo potofu kwamba huenda vurugu hizo
zimechangiwa na baadhi ya wanasiasa jambo ambalo si kweli kwani jeshi la
polisi linaamini kuwa kundi hilo la uhalifu halina itikadi yoyote ya
siasa.
“Polisi
inawashikilia watu hao kwa tuhuma za uhalifu na ninaamini watu hawa ni
wahalifu hivyo watafikishwa mahakani kwa makosa ya uhalifu tu na wala
hakuna siasa,”alisema
Hata
hivyo aliwataka walimu pamoja na viongozi wa chama cha walimu kuacha
kuwahamasisha wezao kufanya mgomo kwani wao tayari walitangaza kugoma na
wamegoma hivyo kupita mashuleni na kuwakuta wezao wanafundisha na
kuwalazimisha kugoma ni uvunjifu wa amani hivyo hatua za kisheria
zitachukuliwa zidi yao.
Kwa
upande wao wanafunzi wakiiongea katika mkutano wa hadhara na wamewaomba
walimu kurejea kazini kwani wanaathirika kimasomo kufuatia mgomo wao
hali wakiwa wanajiandaa kufanya mitihani kwa darasa la nne,saba,kidato
cha pili na nne.
Naye,Diwani
wa Kata ya Tunduma kupitia tiketi ya CHADEMA mheshimwa Frank
Mwakajoka,amesema hujuma zilizofanywa na vibaka hao hali hiyo
haitavumiliwa na kuwataka wakazi wa mji huo kuwa walinzi wa mali za
umma,kwa kitendo hicho kimefanywa na watu ambao si wakazi wa
Tunduma,hali inayopelekea wakazi kuathirika.
Ameongeza
kwa kusema wale wote waliohusika na uhalifu huo kurudisha vifaa
vilivyoibwa ili huduma ziendelee kama kawaida,ambapo baadhi ya bidhaa
zimeanza kurudishwa na kukabidhiwa Jeshi la Polisi.
0 comments:
Post a Comment