Habari na Ezekiel Kamanga,Mbarali.
Chama
cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA),kimeendelea kujizolea wanachama
wapya baada ya kufanya mkutano wa hadhara Agosti 8 mwaka huu katika
Kijiji cha Kongoro Mswisi,Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya.
Mkutano
huo ulifunguliwa na Mwenyekiti wa chama hicho wilaya Bwana Peter
Mwashite wakiwa na nia ya kutoa shukrani kwa wananchi wa kijiji hicho
waliokipigia kura chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010 wa
kuchangua Rais,Wabunge na Madiwani,licha ya kura kutotosha kukiwezesha
chama hicho kuibuka na ushindi.
Aidha,katika
mkutano huo viongozi kadhaa wa chama hicho walipanda jukwaani na kunadi
sera za chama akiwemo aliyewahi kugombea nafasi ya ubunge wa Jimbo la
Mbarali Bwana Gidawaya Kazamoyo,Diwani wa viti maalumu Lucy
Ngonde,Diwani wa Kata ya Kiwira,Wilaya ya Rungwe Bwana Julius Laurent
Mwakalibule,Mwenyekiti wa Vijana mkoa Bwana Julius Kasambala na
Bi.Agatha John ambaye ni mwenyekiti wa wanawake Wilaya ya Mbeya Mjini.
Katika mkutano huo kadi za wanachama zaidi ya 74 kutokea Chama Cha Mapinduzi(CCM) walijiunga na chama cha CHADEMA.
Akihutubia
mkutano huo Diwani wa Viti Maalumu wa wilaya ya Mbarali Bi, Lucy
Ngonde,amesema kuwa zaidi ya bilioni 1.4 pesa za Halmashauri ya wilaya
hiyo zimefujwa ba kusababisha miradi ya maendeleo kukwama na kwamba pesa
hizo ni tofauti ya shilingi milioni 87 zimefujwa na Mweka Hazina wa
halmashauri hiyo.
Wakat
huohuo amemtaka Mkurugenzi wa wilaya hiyo kutenga bajeti ya fedha kwa
ajili ya chaguzi za vitongoji,ambapo imebainika kuwa baadhi ya vijiji
vina makaimu wenyeviti kikiwemo Kijiji cha Mswiswi,kitongoji cha
Uswafwani hakina mwenyekiti kwa takribani mwezi mmoja mpaka sasa,Majengo
Mapya miaka miwili,Mshikamano miaka mitatu na Maendeleo miaka
miwili,hali inayopelekea kuzorota kwa maendeleo wilayani humo.
0 comments:
Post a Comment