Na Ester Macha,Mbeya.
Wamiliki
wa makampuni ya ununuzi wa zao la pareto Mkoani Mbeya wametakiwa
kufuata taratibu zilizowekwa katika ununuzi wa zao hilo ili kuwanufaisha
wakulima badala ya kujinufainisha wamiliki pekee.
Mtakwimu
wa bodi ya pareto Nyanda za juu kusini ,Tumaini Ngojile amesema ni vema
makampuni yanayojishughulisha na ununuzi wa pareto kufuata taratibu
zote zilizowekwa ili kuweza kupata mzazao bora kwa faida ya kulima
ambaye kwa kiasi kikubwa ndiye anayeumia.
Ametaja
taratibu hizo kuwa ni mnununuzi kuhakikishe ana leseni ya kazi, lazima
anunue pareto inayoletwa kituoni na siyo kwenda majumbani kununua.
Aidha
amesema wanunuzi wanatakiwa kutekeleza makubaliano yao kwa kuweka vibao
vya majina ya makampuni na bei rasmi za ununuzi kwa siku husika ya
soko.
Hata
hivyo Ngojile amehimiza mizani zinazotumika zikaguliwe kabla ya kwenda
kufanyia kazi ili kuepuka udanganyifu unaweza kufanywa na
wanunuzi,alipiga maarufuku kununua pareto mbichi kwani inalenga
kuzooretesha ubora wa zao hilo.
Aidha
ametoa wito kwa wakulima na makampuni, wakulima wasikubali kuuza pareto
kwa walanguzi kwani lengo lao siyo la kibiashara na badala yake
wanalenga kuzoretesha zao hilo na kwamba makampuni yatakayobainika
yanalangua na kununua pareto majumbani sheria kali zinachukuliwa.
0 comments:
Post a Comment