*Ni baada ya tuhuma za ubadhilifu wa shilingi 180,000/=H
*Akiri kuzilipa mkutanoni pesa anazodaiwa.
*Mjumbe wa Halmashauri ajimegea shilingi 424,400/=
Habari kamili na Ezekiel Kamanga,Mbarali.
Mwenyekiti
wa Kijiji cha Azimio Mswisi,Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya Bwana Luka
Mwanyangwa amelazimika kujiuzuru pamoja na Halmashauri ya kijiji hicho
baada ya kukiri kufuja pesa za kijiji hicho jumla ya shilingi
180000,zilizokuwa zimetolewa na mradi wa TASAF kwa ajili ya ujenzi wa
Zahanati ya kijiji hicho.
Mjumbe
wa Halmashauri hiyo Bwana Daud Ngwale,anahusishwa kufanya ubadhilifu wa
shilingi 424,400 ambapo inadaiwa kuzichukua fedha hizo katika akaunti
ya kijiji na kuamua kuzitafuna badala ya kuzielekezea katika mradi
uliokusudiwa.
Aidha,katika
mkutano uliofanyika kijijini hapo Agosti 4 mwaka huu ulipobainika
ufujaji huo na uliazimia viongozi hao kurejshewa pesa hizo mara moja
vinginevyo wangefungwa kamba na kupelekwa Polisi ambapo Mwenyekiti Bwana
Mwanyangwa alizilipa papo hapo shilingi 180,000 na kutangaza kujiuzuru
uongozi huku mwenzake Bwana Ngwale akipewa muda hadi 1gosti 9 mwaka huu
awe amezirejesha pesa hizo.
Hata
hivyo Afisa Mtendaji wa kijiji hicho Bwana Tito Gerald Joha,amekiri
kupokea pesa kutoka kwa mwenyekiti huyo wa kijiji na kujiuzuru kwake
anatarajia kutoa muhtasari wa mkutano huo na kuwasilisha kwa Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali kwa maamuzi zaidi.
Wakati
huo huo,mbali na ubadhilifu huo,halmashauri hiyo imetumia zaidi ya
shilingi 200,000 kwa ajili ya kuendesha kesi ya Bwna Robert
Mwaigwisa,ambapo rai imetolewa kwa wote waliofanikiwa kwa wananchi
kutojichukulia hatua ya kisheria.
0 comments:
Post a Comment