Pages


Home » » ULEVI WA KUPINDUKIA WAMSABABISHIA MWALIMU KULALA MSALANI.

ULEVI WA KUPINDUKIA WAMSABABISHIA MWALIMU KULALA MSALANI.

Kamanga na Matukio | 04:50 | 0 comments
*Ni katika sherehe za Nanenane,wasamaria wema wamwokoa.
Habari na Ezekiel Kamanga,Chunya.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida kwa kioo cha jamii,Mwalimu Timotheo Samaitu wa Shule ya Msingi Magamba,Kata ya Magamba,Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya,alipoiacha familia yake majira ya saa sita mchana Agosti 8 mwaka huu kisha kulala katika Choo kibovu kwa kile kinachodaiwa na ulevi wa kupindukia.

Mwalimu huyo alitoa kali ya mwaka aple alipoenda kulala katika Kilabu cha Pombe za kienyeji,majira ya mchana na kuamua kuuchapa usingizi fofofo mpaka pale alipoamshwa na watu wasamaria wema.

Watu hao ni pamoja na Kasimu Lupa,Safari Hemson,Mashaka Ilonje na Rafael Andson kwa pamoja walimbeba mwalimu huyo kutoka katika choo cha kilabu hadi nyumbani kwake huku mwalimu huyo akiwa hajitambui.

Mwalimu Samaitu,ambaye pia ni Mwalimu Mkuu msaidizi imedaiwa kuwa amekuwa na tabia ya ulevi wa kupindukia,hali inayodhalilisha taaluma nzima ya Ualimu nchini.

Aidha,taarifa hizo zilifikishwa kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji Bwana Fabian John,ambaye amethibitisha taarifa hizi,pia Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mtakuja Bwana Bahati Athuman Mtwale kwa upande wake amewashukuru wananchi waliotoa masaada wa kuokoa maisha ya mwalimu huyo kutokana na ubovu wa choo hicho.

Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger