Na Esther Macha,Mbeya
Wakati
vugu vugu la uchaguzi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)likiendelea
kushika kasi Rais wa Chama wakandarasi Wenyeji Tanzania(TLCO)Bw.Kura
Mayuma amechukua fomu ya kugombea nafasi ya Uenyekiti wa Mkoa wa Chama
hicho Mkoani Mbeya.
Alisema kuwa lengo ni kushawishi serikali kukataa sheria na kanuni kandamizi kwa wananchi ambazo zimetungwa na Bunge n a mabaraza ya madiwani Mkoani hapa.
Bw.
Mayuma alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari
mara baada ya kuchukua fomu za kugombea nafasi hiyo katika Ofisi za
chama cha mapinduzi zilizopo eneo la Sokomatola.
Alisema kuwa lengo la kugombea nafasi hiyo ni kutaka kurudisha hadhi ya chama hicho Mkoani
hapa ambacho tayari kimeppoteza mvuto kwa wanachama wake ili mwaka 2014
wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa uwe rahisi kupata viongozi
wenye sifa.
“Pia katika uchaguzi huu kutawezesha kupata viongozi wenye sifa kwa uchaguzi wa mwaka 2015 kwani tayari tutakuwa tumepata viongozi wenye sifa ya kuongoza na hapa nimewingia kwa makusudi ili kuweza kukinusuru chama cha mapinduzi “alisema.
Alisema watu wanachaguliwa katika chama watekeleze matakwa ya wananchi badala yake wanashindwa kufanya yale waliyoagizwa na hivyo kuanza kutokea vurugu za wamachanga ambayo chanzo chake ni watendaji wa chini na hivyo CCM kuonekana kushindwa kuwajibika kwa wananchi.
Bw.
Mayuma alisema hiyo inatokana na watendaji wa serikali kushindwa
kuwajibika ,sera ya chama cha mapinduzi ni nzuri ila watendaji wake ndo
wamekuwa tatizo kubwa.
Kwa
Upande wake Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoani mbeya Bw. Maganga
Sengelema alisema kwa sasa chama hicho kinajipanga vizuri ili kuweza
kupata viongozi ambao watakitetea chama tawala katika uchaguzi wa
serikali za mitaa mwaka 2014.
0 comments:
Post a Comment