Habari na Ester Macha,Mbeya.
Kutokana
na waandishi wa habari wanawake nchini kutojikita zaidi katika
uandishi wa habari za wanawake imeelezwa kuwa hali hiyo imesababisha
habari zinazohusu wanawake kutoripotiwa kwa undani zaidi na badala yake
waandishi wa habari wanaume ndio wamekuwa wakiandika habari hizo.
Waandishi
wa habari wanawake ndo wanatakiwa kuwa nguzo muhimu katika kuandika
habari za afya hususani wanawake waliopo vijijini,wengi wanafahamu
matatizo ya wanawake hivyo itakuwa rahisi kuripoti habari hizo kwa
upana .
Mwito huo umetolewa jana na Mkufunzi wa wa mafunzo ya habari za afya Dkt.Ahmed Twaha wakati akitoa mada kwa waandishi wa habari wanaohudhulia mafunzo hayo ya siku nne ambayo yanaendeshwa na umoja wa clabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC).
“Nyinyi kama waandishi wa habari wanawake mnatakiwa kuwa wa kwanza kuandika
habari za afya kutokana na kuwa na uelewa zaidi kuhusu masuala ya
wanawake kwa maradhi mbali mbali ambayo wanaugua,kwa uelewa wenu mtaweza
kuandika kitu ambacho ni kizuri”alisema.
Alisema
mara nyingi waandishi wa habari wanaume ndio wamekuwa wakiandika zaidi
habari za afya tofauti na wanawake wenyewe ambao wana uelewa zaidi ,kuna
umuhimu wanawake kuanza rasmi kujikita zaidi na uandishi wa habari hizi
za afya.
Aidha Dkt.Twaha alisema kuwa wakati wa kuandika habari za afya ni muhimu kuandika kwa takwimu sahihi ili jamii iweze kupata taarifa ambayo imefanyiwa utafiti wa kina na kuelewa nini kinazungumzwa.
Hata Mkufunzi huyo alisema pia kuna umuhimu kuangalia changamoto zinazowakabili wanawake
waliopo vijijini kuhusiana na huduma za afya,na kwamba asilimia kubwa
ya wanawake na watoto ndio wanaotibiwa katika hospitali kuliko wanaume.
Kwa upande wao waandishi habari wanawake wanaohudhulia mafunzo ya habari za afya walisema kuwa wanashindwa kuandika habari hizo kutokana na kutokuwa na vitendea kazi pamoja na uwezeshaji wa kifedha kutokana na habari nyingi kuwa vijijini .
Mafunzo
hayo yanaendeshwa na umoja wa clabu za waandishi wa habari Tanzania
(UTPC)na yanajumuisha waandishi 18 kutoka Mkoa wa Mbeya.
0 comments:
Post a Comment