Na Bosco Nyambege ,Mbeya.
Mwitikio wa watu katika matumizi ya huduma ya ARV Mkoani Mbeya umebainika kuwa ni mkubwa.
Hayo
ni kwamujibu wa kaimu mratibu wa kitengo cha UKIMWI mkoa wa Mbeya
Dkt.Francis Philly alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini
kwake jumatano hii.
Philly amesema
kuwa mwitikio wa wagonjwa wanaotumia dawa za ARV kuwa ni mkubwa kwani
takwimu zinaonesha kuwa kuanzia June 2004 hadi June 2012 wagonjwa
waliojiandikisha katika huduma ni 106598 ambapo watu wazima ni 92085 na
watoto ni 12889.
Ameongeza
kuwa kati ya hao walioanzishiwa dozi ya ARV ni 52903 ambapo watu wazima
ni 40701 na watoto ni 12202 na watu 13163 hawajulikani kama wamekatisha
dozi ama wameacha na katika hospitali ya mkoa wa mbeya watu 7675
wameandikashwa na 3539 wameanzishiwa tiba ya ARV na watu 1766
hawajulikani walipo na hali hii inaonesha wazi kuwa watu hawafuati
maelekezo ya wataalamu wa afya .
Kwa takwimu hiyo inaonyesha kuwa zaidi ya 50%ya watu wote ambao wameandikishwa katika huduma CTC wameanzishiwa dawa.
Kwa
upande wake Afisa muuguzi wa kitengo cha CTC katika Hospitali ya mkoa
wa Mbeya Mariam Mhanjo amesema kuwa katika sekta hiyo wanakabiliwa na
changamoto mbalimbali kama vile ukosefu wa vitendea kazi, upungufu wa
wahudumu katika sekta hiyo,miundombinu mibovu hususani vijijini pamoja na masilahi kuwa duni.
Hivyo Mhanjo ameiomba serikali kuweza kuwasaidia kutatua changamoto hizo ili kuweza kufanya kazi katika mazingira mazuri na yanayorizisha.
0 comments:
Post a Comment