Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Upungufu wa vifaa katika kitengo cha Maabara katika hospitali ya Mkoa wa Mbeya umetajwa kuwa changamoto kubwa ambayo inapelekea wagonjwa kuwa katika wakati mgumu wa kupata vipimo muhimu .
Hayo yalisemwa jana na Mratibu wa Huduma za Maabara katika hspitali ya Mkoa wa Mbeya Dkt.Ezekiel Tuya wakati alipozungumza na gazeti hili kuhusu matatizo ambayo yanakwamisha shughuli za maabara hosptalini hapo.
Alisema ukusefu huo wa vifaa unasababisha kuendelea kudorola kwa huduma , na tatizp kubwa lingine ni upungufu wa wataalamu katika taaluma ya afya hasa vitengo vya maabara katika hospitali hiyo ambapo hali hiyo inasababisha wanafdunzi kuyakimbia masomo ya sayansi ambayo ndiyo msingi wa afya.
“Hili
ni tatizop kwani mara nyingi wanafunzi wanaotaka kuja kufanya mazoezi
wanashindwa kutokana na kutokuwa na kutokuwa na wataalamu wa hivyo ni
jambo ambalo ni muhimu ambali serikali inatakiwa kulifanyia kazi , na
hata huu ukosefu wa vifaa nao unatutesa sana hasa ukizingatia kipindi
hiki ambacho tuna wagonjwa wengi ambao wanahitaji vipimo ili waweze
kuazishiwa matibabu ya dawa”alisema.
Alisema tatizo linguine ukosefu wa vifaa wa vifaa na vitendanishi katika maabara vifaa ambavyo hurahisisha utendaji wa kazi kwa watumishi wa maabara.
Hata hivyo Dkt. Tuya ameiomba serikali kushughulikia ukosefu wa wataalamu wa maabara nchini ili kunusuru maisha ya watanzania wanafariki dunia kwa kukosa huduma ya vipimo kwa wakati .
0 comments:
Post a Comment