Pages


Home » » SERIKALI YAOMBWA KUTOA USHIRIKIANO KWA MASHIRIKA BINAFSI.

SERIKALI YAOMBWA KUTOA USHIRIKIANO KWA MASHIRIKA BINAFSI.

Kamanga na Matukio | 04:37 | 0 comments
Na Bosco Nyambege,Mbeya
Serikali imeombwa kutoa ushirikiano ipasavyo kwa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali(Binafsi) nchini yanayofanya kazi ya kutoa misaada kwa wananchi waishio katika mazingira magumu na hatarishi.

Hayo yamesemwa na mchungaji Israel Ernest wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii nje kidogo ya ukumbi wa maktaba ya Mkoa wa Mbeya mara baada ya semina ya ujasiriamali iliyokuwa ikifanyika maeneo hayo.

Amesema kuwa kwani wananchi wanaoishi katika mazingira magumu wanaweza kutoka katika hali hiyo kwa msaada wa Serikali kwa kushirikiana na watanzania walio na uchungu wa kimaisha kwa kuwafundisha kutumia rasilimali walizonazo.

Mchungaji Ernest ameongeza kuwa wapo wajasiriamali wanaotamani kufika vijijini lakini wanashinda kutokana na miundombinu mibovu na kama serikali itawasaidia kuwarekebishia hali hiyo wanaweza kufika mpaka huko na kuwaokoa wananchi hao.

Kwa upande wake Bi. Agnes Lyuki ambaye ni miongoni mwa wakufunzi wa semina hiyo amewasihii watanzania kuweza kujifunza kwa wale walioendelea kimaisha na si kujifunza kwa yule aliye feli kimaisha.

Kwa upande wa wananchi waliopata wasaa wakuzungumzia suala hilo wao wameiomba serikali kuweza kufanya haraka sana kurekebisha miundombinu kama barabara ili kuwawezesha wananchi waishio vijijini kuweza kufikiwa a semina mbalimbali ambazo mara nyingi zinaishia mijini.

Pia wameiomba Serikali na mashirika ya kifedha kuweza kuwasaidia mitaji wananchi waishio vijijini ili kuweza kujikwamua kiaisha na kuachana na suala la umasikini unaowakumba.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger