Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Wananchi wa Tarafa ya
Itaka inayojumuisha kata ya Bala, Halungu, Itaka na Nambizo, wilayani
Mbozi wamekataa kukatwa shilingi 200 toka kwenye mauzo yao ya kahawa
kwa ajili ya kuchangia hisa ya uanzishwaji wa benki ya wananchi wa
wilaya humo.
Katika
mkutano wa baraza la madiwani uliofanyika wilayani hapo uliazimia kila
mkulima kukatwa shilingi 200 toka katika mauzo yao ya kahawa ambapo
madiwani hao baadhi yao walionekena kutofautiana na kauli ya Charles
Chenza, ambaye ni mwaandaji wa rasimu ya uanzishwaji wa benki ya
wananchi wilaya ya Mbozi ambapo alisema kuwa kila mkulima wa zao hilo
atakatwa kiasi hicho cha fedha ili kuchangia hisa ya benki hiyo.
Kufuatia
kauli hiyo ya Chenza, wananchi tarafa hiyo waliamua kuitisha mkutano
wa ndani agosti 18 mwaka huu katika kata ya Halungu ukihusisha madiwani
toka kata zote za tarafa hiyo, na vikundi 24 vinavyohusika na ununuzi
wa kahawa ambapo kwa pamoja walipinga kauli hiyo.
Wananchi hao walisema walifikia uamuzi huo wa kupinga kwa madai yakuwa hawakuwashirikishwa katika kikao chochote na kukubaliana na maamuzi hayo kwani suala la ununuzi wa hisa ni hiari ya mtu na kwamba walisema kuwa wao hawapingi kuanzishwa kwa benki hiyo.
Eribariki
Msukwa, mkazi wa Nambizo, alisema kuwa wananchi wa wilaya hiyo
wamekuwa wakionewa mara kwa mara kwa kukatwa fedha zao za mazao
hususani zao la kahawa na fedha hizo kutokuwa na maelezo ya kutosha
huku serikali ikishindwa kuwasaidia.
Alisema
kuwa baada ya kikao hicho waliazimia kuunda kamati itakayokwenda
kumuona mkuu wa wilaya hiyo Dr. Michael Kadeghe, mkuu wa Mkoa wa
Mbeya,Abbas Kandoro na hatimaye kwenda Bodi ya Kahawa(TCB) Moshi ili
kupinga kwa ukatwaji wa fedha hizo.
Aidha,
walisema kuwa endapo itashindikana kupata msaada toka kwa viongozi hao
wanaokusudia kuwafuata basi wataamua kwenda moja kwa moja mahakamani
ili kudai haki yao.
Hata
hivyo madiwani wa kata hizo kwa pamoja walionekana kupingana na kauli
iliyotolewa na mwandaaji wa rasimu ya uanzishwaji wa benki hiyo,Charles
Chenza ndani ya kikao hicho ambapo hata baada ya hapo madiwani hao
waliweza kukaa na wanachi wao ili kuwapa taarifa na ambapo waliamua kwa
pamoja kupinga suala hilo.
Madiwani hao ni pamoja na Wiston
Songa,toka kata ya Bara, Alan Mgula toka kata ya Itaka, Samson Simkoko
toka kata ya Halungu,Bernad Mweniyonde wa kata ya Nambizo, na Salome
Kibweja diwani viti maalum.
Katika
kamati hiyo walioteuliwa ni Eribariki Msukwa toka kata ya Nambizo,
Cairo Msyete wa kata ya Bara, Taji Mwashambwa wa kata ya Itaka na Lewadi
Sikaponda wa kata ya Halungu.
Wakati
huohuo baada ya kumkosa Mkuu wa wilaya ya Mbozi,walimuona Mkurugenzi wa
halmashauri ya wilaya hiyo Bwana Levson Chileo amekiri kufanyika makosa
hayo na hivyo amewataka wakulima hao kwenda Moshi Mkoani
Kilimanjaro,kuiona bodi ya kahawa nchini TCB ILI kuzuia ukatwaji wa pesa
hizo.
Wajumbe waliofanikiwa kuondoka ni pamoja na Bwana Eribariki Msukwa na Leward Sikaponda.
0 comments:
Post a Comment