Pages


Home » » HITILAFU YA UMEME YASABABISHA VIFO VYA MWANAMKE MMOJA NA WANAWE WAWILI.

HITILAFU YA UMEME YASABABISHA VIFO VYA MWANAMKE MMOJA NA WANAWE WAWILI.

Kamanga na Matukio | 03:04 | 0 comments
 Sehemu ya masalia ya vyombo na samani zilizoteketea kwa moto kufuatia hitilafu ya umeme iliyopelekea mama mmoja na wanawe wawili nao kutoketea katika Mtaa wa Mapelele,Kata ya Ilemi Jijini Mbeya.
Nyumba iliyoteketea kwa moto baada ya hitilafu ya umeme.(Picha zote na Ezekiel Kamanga)
*******
Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Mwanamke mmoja mkazi  wa mtaa wa Mapelele kata ya Ilemi Jijini Mbeya amefariki dunia akiwa amelala chumbani  na wanawe wawili baada ya moto mkubwa kuzuka uliosababishwa na hitilafu ya umeme majira ya saa 4.55 usiku agosti 16 mwaka huu wakati familia hiyo ikiwa imelala chumbani .

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Bw. Barakiel Masaki aliwataja marehemu hao kuwa ni pamoja na Bi.Pendo Paul (23) mkazi wa Ilemi, na watoto wake wawili ambao ni Tekla Paul(4),Aman Paul mwaka mmoja ambao wote walikuwa wamelala chumba kimoja wakati moto unatokea.

Alisema kuwa wakati moto huo unatokea mume wa mwanamke huyo aitwaye Paul Mlelwa alikuwa safarini Jijini Mwanza kikazi kwa muda wa wiki moja sasa toka aondoke na kwamba familia hiyo imehamia katika nyumba hiyo  ya kupanga  mwezi mmoja uliopita.

Akizungumzia tukio hilo barozi wa mtaa huo Bw.Pius Mwampenjele alisema alipata taarifa za ajali ya moto huo ndipo alipoomba msaada kwa majirani ili kuweza kusaidia kuzima moto ambao tayari ulikuwa umeshateketeza vyumba viwili  na familia ya Bw. Paulo ambayo ilikuwa na mke na watoto wawilli waliokuwa wamelala chumbani walishafariki dunia.

Hata hivyo Mwenyekiti wa mtaa wa Mapelele Bw.Christopher Mwakibete alisema kwamba tukio hilo  ni la pili katika mtaa wake kwa muda wa wiki moja  kufutia tukio la kwanza kutokea agosti 14 mwaka huu ambapo watu wawili ambao ni mke na mume walifariki dunia kwa moto uliosababishwqa na hitilafu ya umeme ambayo ilikuwa ni majira hayohayo.

Alisema kuwa matatizo ya umeme katika mtaa wake yamelipotiwa mara nyingi kwa diwani wa kata ya Ilemi na ofisi za Tanesco Mkoa lakini hakuna hatua zozote ambazo zimechukuliwa  zaidi ya kutelekeza nguzo za umeme kwa muda mrefu bila utekelezaji .

Aidha ameongeza kuwa uwezo Transifoma umekuwai mdogo kutokana  na wingi wa wateja na mara nyingi umeme umekuwa mdogo na wakati mwingine kuzima kabisa hali ambayo inahatarisha usalama wa wananchi wa eneo hilo.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger