Pages


Home » » MKUU WA MKOA WA MBEYA Mh. KANDORO AZINDUA KAMATI YA MAFANIKIO YA ULINZI NA USALAMA MKOA.

MKUU WA MKOA WA MBEYA Mh. KANDORO AZINDUA KAMATI YA MAFANIKIO YA ULINZI NA USALAMA MKOA.

Kamanga na Matukio | 05:46 | 0 comments
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Abbas Kandoro akipokea taarifa kutoka kwa Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa Advocate Nyombi ofisini kwake kuhusu mpango wa Kamati ya mafanikio ya kuimarisha Ulinzi na Usalama mkoani hapa.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mbeya Advocate Nyombi akitoa maelezo kwa Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Abbas Kandoro ofisini kwa mkuu wa mkoa kuhusu mpango wa Kamati ya mafanikio ya kuimarisha Ulinzi na Usalama mkoani hapa.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Abbas Kandoro(mwenye suti nyeusi) katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya ya mafanikio ya kuimarisha Ulinzi na Usalama mkoani hapa.
Mwenyekiti wa Kamati ya mafanikio ya kuimarisha Ulinzi na Usalama Bwana Julius Kaijage akitoa shukrani baada ya kupewa wadifa huo katika Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Abbas Kandoro.
 *****

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Abas Kandoro azindua kamati ya mafanikio ya ulinzi wa na usalama kwa mkoa wa Mbeya ambayo inahusisha wafanyabiashara, viongozi wa dini na kimila.

Akitoa taarifa mbele ya mkuu wa Mkoa Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi amesema madhumuni ya kamati hiyo ni kusaidiana na jeshi la polisi ili kuleta amani mkoani hapa na wajibu wa kuelimisha wananchi kuhusu amani, na kwamba pasipo amani hakuna maendeleo hivyo ni kila wajibu wa kila mwananchi kuhimiza amani.

Walioteuliwa ni Bwana Julius Kaijage ambaye ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Makamu mwenyekiti ni Forbet Kyando, Katibu ni Bi Mary Haji Nkembo, Mjumbe ni Bwana Basilio Mwaliojo, Shehe Dulu Issa, Shayo Masoko, Binti Balema, Greyson David.

Kamanda Nyombi anaingia katika kamati hiyo akiwa na askari wake Majaliwa Mbogela na Moses Semindu.

Hata hivyo pamoja na majukumu mengi kamati hiyo itakuwa na wajibu wa kujenga vituo vya polisi ili kusogeza karibu huduma za kipolisi na kudumisha amani na kuimarisha dhana ya polisi jamii na ulinzi shirikishi.

Akiongea baada ya kusimikwa wadhifa Mwenyekiti wa kamati hiyo Bwana Julius Kaijage amesema kuwa wadau wenyekupenda maendeleo wawe tayari kuichangia kamati hiyo na kutoa mawazo yao ili kuendelea kuimarisha ulinzi na amani kwa mkoa wa Mbeya kwani ni mpango wa nchi nzima kuanzisha kamati za mafanikio kwa kila mkoa.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger