Pages


Home » » ZIARA YA KAMANDA WA UVCCM MKOA WA MBEYA YAFANA.

ZIARA YA KAMANDA WA UVCCM MKOA WA MBEYA YAFANA.

Kamanga na Matukio | 05:39 | 0 comments
Ziara ya Kamanda wa vijana UVCCM mkoa wa Mbeya Dr Stephem Mwakajumilo ameibua mambo kadhaa yakifanyiwa kazi UVCCM na Chama cha Mapinduzi kuimarika:-.
1. Novemba 5, Mwaka huu - Wilayani Chunya:- Vijana wakataa taarifa ya kamati ya utekelezaji wadai ilikuwa ya kutengenezwa mezani na sio sahihi, wamcharukia Katibu wa UVCCM wilayani humo na Maji yaanza kutoka kijiji cha Mbuyuni baada ya Ziara hiyo.

2. Novemba 6, Mwaka huu - Wilayani Mbozi:- Halaiki kubwa wampokea Kamanda UVCCM Mkoa Dr Stephen Mwakajumilo, Mwenyekiti wa UVCCM aingia mitini na kuhamasisha vijana kutohudhuria mkutano wa Baraza ili kuficha uovu wake hali ikawa ndivyo sivyo Mkutano wafanyika bila yeye kutokuwepo, Fedha za msaada zilizotolewa Shilingi milioni 2 hazina ya maelezo ya kina na Kamanda ataka kupewa mrejesho wa fedha hizo na misaada mbalimbali iliyotolewa.

3. Novemba 7, Mwaka huu - Wilayani Ileje:-
Baraza la vijana la mlalalamikia Katibu wa UVCCM wilaya kwa kutumia vibaya fedha na pikipiki kwa manufaa yake binafsi, nyimbo za kejeli zaimbwa hatimaye Katibu huyo wa wilaya UVCCM aomba kwenda kusoma, Ofisi ya wilaya yaridhia wanachama wamtaka kutorudi kutokana na kuwagawa wanachama.

4. Novemba 8, Mwaka huu - Wilayani Mbarali:- Katibu wa UVCCM wilaya, aangua kilio baada ya kuhojiwa kutokana na kushindwa kuandaa taarifa ya utekelezaji ya wilaya licha ya mapokezi makubwa. Kamanda wa UVCCM mkoa aingilia kati kuokoa mkutano huo kufanyika kwa utulivu.

5. Novemba 9. Mwaka huu - Wilayani Mbeya Vijijini:- Kamanda wa UVCCM mkoa Dr Mwakajumilo abaini kutokuwepo kwa Kamati ya utekelezaji, Katibu wa UVCCM wilaya aumwa BP ghafla ambapo haikufahamika anapatiwa matibabu katika Hospitali gani na mpaka sasa hajaripoti kituo cha kazi na wala Katibu wake wa mkoa hana taarifa. Mbunge wa jimbo la Mbeya Vijijini Mchungaji Lackson Mwanjale ashindwa kutoa milioni moja kwa ajili ya mradi wa Vijana kama ahadi aliyokuwa ameihaidi.

6. Novemba 10, Mwaka huu - Wilayani Rungwe:- Vijana wa UVCCM wajitokeza kwa wingi kumlaki Kamanda wa UVCCM mkoa Dr Mwakajumilo walalamikia makundi yanayokizana katika kipindi cha kura za maoni, Kamanda awaasa kufanya kazi ipasavyo makundi yamekwisha , afurahisha na taarifa ya utekelezaji wa wilaya hiyo.

7. Novemba 12, Mwaka huu - Wilayani Kyela:- Kamanda wa UVCCM mkoa Dr Mwakajumilo nusura apigwe changa la macho kutokana kubaini mradi hewa wa Soda, taarifa yaonesha UVCCM wilaya wana fedha taslimu milioni 25 za kitanzania, huku wakitaka kuomba msaada wa shilingi milioni 50, kuimarisha mradi huo alipotaka mchanganuo uongozi washindwa kueleza na kukiri kwamba ni uongo. Kamanda awataka viongozi kuwa wawazi na wa kweli.

8. Novemba 13, Mwaka huu - Wilayani Mbeya mjini:- Ziara haikufanyika kutokana na vurugu iliyosababisha kurindima kwa mabomu ya machozi na Ziara hiyo kuahirishwa hadi pale itakapopangwa tena.

9. Novemba 14, Mwaka huu - Wilayani Ileje:- Kamanda wa UVCCM wilaya Ileje Bwana Gideon Cheyo aongoza mapokezi makubwa yaliyopambwa kwa maandamano ya pikipiki, sare za UVCCM zashonwa, Kamanda UVCCM mkoa  Dr Mwakajumilo afuradishwa na mapokezi hayo vijana watakiwa kujiunga katika vikundi vya uzalishaji mali katika kujikomboa na uchumi.

Ziara kama hii ikifanywa na Viongozi mbalimbali zitaimarisha uwajibikaji maeneo ya kazi na kuimarisha uhai wa Vyama nchini na hivyo kukuza uchumi wa nchi badala ya kukaa maofisini.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger