Mwimbaji wa Nyimbo la Injili nchini Tanzania Bi Rose Muhando akiwa ameshika moja ya tuzo alizotunukiwa Mnamo mwaka 2005 Tuzo ya muziki, Tanzania kupitia kipengele cha Mwimbaji bora wa kike na wimbo bora wa dini ( "Mteule uwe macho")
Msanii wa nyimbo za Injili Bi Rose Muhando katika taswira ya kava ya Albamu yake ya tatu inayoitwa Jipange sawasawa iliyoingizwa sokoni mnamo mwaka 2008
*****
Na mwandishi wetu.
Mchungaji wa kanisa la Bethel Kituo cha Mbinguni mchungaji Jonathan Kyando amemtaka mwimbaji wa Nyimbo za Injili nchini Bi Rose Muhando kurejesha pesa zenye thamani ya shilingi 2,500,000/= alizopewa kwa ajili ya kufika mkoani Mbeya kutoa huduma neno la Mungu kupitia nyimbo za Injili katika mkutano wa Injili uliofanyika katika kanisa hilo Novemba 18 hadi 20, mwaka huu.
Mwimbaji huyo alitakiwa ahudumie katika kanisa hilo lililopo eneo la Soweto jijini Mbeya kwa mapatano ya kulipwa kiasi hicho cha pesa ili awezekufika ndipo kanisa hilo likakubali na kumtumia pesa hizo kwa awamu tatu ambapo Octoba 11, mwaka huu alilipwa shilingi milioni moja na laki tano, hali kadharika Novemba 3, mwaka huu alilipwa shilingi lakitano majira ya asubuhi na kumaliziwa laki tano nyingine jioni na hivyo pesa hizo kutimia shilingi milioni Mbili na laki tano.
Hata hivyo baada ya kulipwa pesa hizo Bi Rose aliwasiliana na uongozi wa kanisa hilo na kudai kuwa ameshaanza safari ya kuelekea Mbeya ambapo angefika Novemba 17 majira ya jioni lakini chakushanga zaidi hakuweza kufika na mpaka siku ya Ijumaa Novemba 18 simu yake haikuweza kupatikana.
Siku ya Jumamosi Novemba 19, mwaka huu Meneja wa Bi Rose Muhando aitwaye Bwana Nathan alimpigia Simu mchungaji Jonathan Kyando, kuwa Rose ameshindwa kufika kutoka na kuumwa hivyo angemleta kwa gari ndogo ya kukodi ambapo mchungaji alikubali lakini hata hivyo hakuweza kufika mpaka mkutano huo wa Injili unamalizika.
Hata hivyo kutokana na kushindwa kufika kwa Bi Rose Muhando, Meneja wake ameahidi kurudisha pesa zote ambazo zilichukuliwa kupitia akaunti ya Benki ya Barclays.
Kumekuwa na lawama nyingi zinazomkabili mwimbaji huyo maarufu wa nyimbo za Injili kwani mara kadhaa amekuwa hafiki katika matamasha na mikutano licha ya kulipwa pesa na wahusika.
Mwimbaji mwingine aliyelalamikiwa mkoani Mbeya ni Bi Catherine Kyambiki ambaye anadaiwa kutolipa pesa ambazo alikopa kwa mtangazaji wa kituo kimoja cha redio mwaka jana, na mwimbaji huyo kutorejesha mpaka sasa licha ya kukumbushwa mara kwa mara lakini amekuwa na tabia ya kubadilisha namba za simu kwa kile kilichotafsiriwa kukwepa deni hilo.
Kyambiki alifanya tamasha la mwisho mkoani Mbeya Oktoba mwaka jana, katika mji mdogo wa Tunduma mkoani Mbeya na mpaka sasa hajawahi kurudi mkoani humo.
WASIFU MFUPI WA ROSE MUHANDO.
Rose Mhando ambaye hujulikana pia kwa jina la Rose Muhando;amezaliwa mwaka 1976 katika kijiji cha Dumila, Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro, nchini Tanzania) ni msanii maarufu wa muziki wa injili katika lugha ya swahili katika kanda ya Afrika Mashariki.
Rose,ambaye alikuwa muumini wa dini ya kiislamu,ni mama wa watoto watatu. Mama huyu alidai kuwa akiwa na umri wa miaka tisa alipata maono ya Yesu Kristo akiwa amelazwa. Aliteseka kwa muda wa miaka mitatu,na baada ya hapo alipona na kubadili dini(kuongoka) na kuwa mkristo.
Alianza fani yake ya muziki kama mwalimu wa kwaya inayoitwa Kwaya ya Mtakatifu Maria katika kanisa la kianglikana linaloitwa Chimuli mkoani Dodoma.
MAFANIKIO
Mnamo tarehe 31 mwezi Januari mwaka 2005, Rose Muhando alipata tuzo ya mtunzi bora, muimbaji bora, na tuzo ya msanii mwenye albamu bora ya mwaka wakati wa tamasha la tuzo za kiinjili, 2004.
Mnamo mwezi wa kumi na mbili, 2005, alishiriki katika tamasha la kiinjili ili kusaidia kutafuta fedha kwa ajili ya kituo cha watoto yatima cha Dar es salaam.
Baadhi ya albamu zake ni pamoja na:
1.Kitimutimu.
2.Uwe Macho, 2004.
3.Jipange Sawasawa, 2008
4.Utamu wa Yesu 2011

TUZO
Mnamo mwaka 2005 Tuzo ya muziki, Tanzania: Mwimbaji bora wa kike na wimbo bora wa dini ( "Mteule uwe macho")

"Rose Mhando atia fora kwenye tamasha la Nane Nane", 2004-08-14. Retrieved on 2007-05-12.
"Mtanziko wa umaarufu wa Rose Mhando", 2005. Retrieved on 2007-05-12.
0 comments:
Post a Comment