RAIS JAKAYA KIKWETE AKIKATA UTEPE KATIKA HOSPITALI HIYO YA MBALIZI IFISI KUASHIRIA KUIFUNGUA RASMI BAADA YA SERIKALI KUUNGANA NA KANISA LA UINJILISTI TANZANIA, NA MKURUGENZI WA MAENDELEO YA KANISA HILO MCHUNGAJI MARKUS LEHNER(KULIA).
*****
Na mwandishi wetu
Hospitali teule ya wilaya ya Mbeya Ifisi, inayomilikiwa na kanisa la Uinjilisti Tanzania iko hatarini kufungiwa kutokana na hospitali hiyo kutokuwa na maji ya kutosheleza.
Uchunguzi uliofanywa kwa muda wa miezi mitano sasa, umebaini kuwa Hospitali hiyo inapata lita 500 badala lita 1000 ambazo zinahitajika kwa siku hospitalini hapo.
Aidha uchunguzi wetu umebaini kuwa wakati hospitali hiyo ikikabiliwa na tatizo hilo la maji mamlaka zinazohusika zimeelekeza kiasi kikubwa cha Maji katika viwanda vilivyopo Jijini Mbeya vikiwemo viwanda vinavyozalisha vinywaji Moto na baridi.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Kanisa hilo la Uinjilisti Tanzaia Mchungaji Markus Lehner amekiri kuwepo kwa tatizo la maji katika hospitali hiyo licha ya hospitali hiyo kuhudumiwa na Serikali.
0 comments:
Post a Comment