Wajasiriamali mkoani Mbeya kunufaika na mafunzo ya siku tatu ya ujasiriamali yatakayotolewa na kampuni ya Dimod Integrated Solution and Awareness kuanzia siku ya Jumatatu Novemba 28 hadi Novemba 30, mwaka huu siku ya Jumatano, Pichani ni gari ya matangazo ya kampuni hiyo likiwa eneo la Kadege jijini Mbeya jana likitoa matangazo ya mafunzo hayo yatakayotolewa katika Ukumbi wa Mkapa jijini hapa.
Kampuni inatotoa mafunzo ya ujasiriamali Tanzania ya Dimod Integrated Solution and Awareness , sasa ipo jijini Mbeya kwa ajili ya semina itakayoendeshwa kwa siku tatau kuanzia jumatatu Novemba 28, mwaka huu.
Mafunzo yatakayotolewa na kampuni hiyo ni pamoja na utengenezaji wa Sabuni ya unga, sabuni ya miche, sabuni ya magadi, sabuni za kuogea, sabuni ya majivu, sabuni za maji, shampoo aina zote, mishumaa aina yote, mafuta ya kupakaa, Lotion, maji ya betri, tomato sourcw, chili source, unga wa lishe, wine aina zote, encubeter, biogas, air fresher, bleach, skin scrub, peanut butter, mango pickle, carpet cleaner, window cleaner, tiles cleaner, stain remover na uyoga.
Masomo ya mifugo na biashara , kutengeneza vyakula vya mifugo na ufugaji bora. Semina itafanyika katika ukumbi wa Benjamini Mkapa Conference Center. Fomu shilingi 2,000 na ada ya mafunzo ni shilingi 10,000 kwa masomo yote ya nadharia na vitendo kuanzia majira ya saa 3 kamili asubuhi mpaka saa 8:30 mchana.
Wakufunzi wa mafunzo hayo ya ujasiriamali ni Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Dr Didas Lunyungu na Bwana Mohammed Omary ambaye ni Mkurugenzi wa mafunzo na kesho wanatarajia kukutana na Mkuu wa wilaya ya Mbeya Bwana Evans Balama majira ya saa mbili asubuhi kujadili mambo mbalimbali namna ya kuwawezesha wakazi wa mkoa wa Mbeya kunufaika kibiashara.na uchumi.
0 comments:
Post a Comment