Pages


Home » » KIJANA NURDIN JUMA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLIZI MKOA WA MBEYA KWA TUHUMA ZA KUSABABISHA MAUAJI YA ASKALI PC AMBROSI

KIJANA NURDIN JUMA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLIZI MKOA WA MBEYA KWA TUHUMA ZA KUSABABISHA MAUAJI YA ASKALI PC AMBROSI

Kamanga na Matukio | 04:53 | 0 comments
Na Ezekiel Kamanga.
Kijana Nurdin Juma mwenye umri wa miaka 27 mkazi wa kijiji cha kibaoni kitongoji cha maili tano wilayani Chunya anashikiliwa na Jeshi la polisi mkoa wa Mbeya kwa tuhuma za kushambulia na kusababisha mauji ya askari PC Ambrosi wa kituo cha polisi wilayani humo.

Habari zaidi zinadai awali mtuhumiwa alikuwa amelewa akiwa ndani ya baa ya Uzunguni ambapo baada ya muda mtuhumiwa JUMA lianza kufanya fujo zilizopelekea wahudumu wa baa hiyo kutoa taarifa polisi ambo nao walifika muda mfupi kwa ajili ya kumdhibiti.

Hata hivyo wakati wakitaka kumdhibiti kijana huyo alimshambulia PC AMBROSI kwa kumpiga kichwa kichwani hali iliyompelekea kupata maumivu makali na kufari kdunia wakati akikimbizwa katika hospitali ya wilaya kwa ajili ya matibabu zaidi.

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Anecletus Malindisa amesema kuwa mwili wa PC AMBROSI umehifadhiwa katika hospitali ya wiulaya Chunya na mtuhumiwa anatarajia kufikishwa mahakamani siku yoyote kujibu tuhuma zinazomkabili.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger