Pages


Home » » ABIRIA 25 WANUSURIKA KATIKA AJALI MKOANI MBEYA

ABIRIA 25 WANUSURIKA KATIKA AJALI MKOANI MBEYA

Kamanga na Matukio | 05:23 | 0 comments
 Baadhi ya majeruhi akiwemo Bi Philomena Fredy (aliyeketi chini) mara baada ya kutoka ndani ya gari ya abiria aina ya Costa yenye nambari za T 621 BQH wakisubiri msaada wa kwenda Hospitali kupewa huduma ya kwanza baada ya gari yao kugongana na gari ya mizigo aina ya Scania yenye nambari za usajili T 783 ATQ eneo la Kalasha wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya jana majira ya saa moja usiku.
 Mmoja wa abiria akitoa mizigo yake ndani gari ya abiria aina ya Costa yenye nambari za T 621 BQH baada ya gari yao kugongana na gari ya mizigo aina ya Scania yenye nambari za usajili T 783 ATQ eneo la Kalasha wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya jana majira ya saa moja usiku.
 Askari wa Jeshi la polisi akipokea maelezo kutoka kwa mmoja wa abiria wakati wakisubiri kupelekwa Hospitalini mara baada ya kutokea kwa ajali baina ya  gari ya abiria aina ya Costa yenye nambari za T 621 BQH kugongana na gari ya mizigo aina ya Scania yenye nambari za usajili T 783 ATQ eneo la Kalasha wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya jana majira ya saa moja usiku.
 Gari ya mizigo aina ya Scania yenye nambari za usajili T 783 ATQ iliyosababisha ajali kwa kugongana na gari ya abiria aina ya Costa yenye nambari za usajili T 621 BQH eneo la Kalasha wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya jana majira ya saa moja usiku.
***** 
Na Ezekiel Kamanga, Mbozi.
Watu ishirini na tano wamenusurika kufariki dunia kufuatia ajali iliyotokea jana majira ya saa moja usiku eneo la Karasha wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya baada ya kugongana kwa magari mawili ilikiwemo gari la abiria aina ya Costa yenyenambari za usajili T 621 BQH na gari ya mizigo aina ya Scania yenye nambari za usajili T 783 ATQ.

Mtandao huu umeweza kushuhudia ajali hiyo ambapo gari ya mizingo ilikuwa ikiendeshwa na dereva aitwaye Egno Ignas mwenye umri wa mika 27 mkazi wa Makambako likitokea Mji mdogo wa Tunduma lilionekana kuyumba barabarani na hivyo kupoteza mwelekeo wa dereva wa Costa aliyekuwa katika hali ya mwendokasi nayo ikitokea Tunduma, ambapo dereva wa Costa alipojaribu kulikwepa gari la mizigo na kuligonga kwa mbele hali iliyosababisha costa kupoteza mwelekeo na kuupalamia mashamba.

Akizungumza na mtandao huu mmoja wa abiria Bi Philomena Fredy amesema gari ya mizigo ilikuwa mbele yao na dereva alipojaribu kulikwepa abiria wakasikia kishindo kikubwa na kufumba na kufumbua wakashituka gari lao la abiria lipo pembezoni mwa barabara baada ya kuparamia matuta.

Majeruhi wote walikimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi na wengine katika hospitali ya Mbozi Mission inayomilikiwa na kanisa la Moraviani Jimbo la Kusini Magharibi.

Hata hivyo polisi walifanikiwa kufika mapema eneo la tukio na kuchukua maelezo ya Utingo wa gari ya mizigo Bwana Godi Mlingo mwenye umri wa miaka 21 ambapo alisema gari yao ilizima ghafla na kupoteza mwelekeo.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger