Mbunge wa jimbo la Mbarali Mwalimu Kilufi(katikati), akisalimiana na baadhi ya wananchi nje ya mahakama ya Hakimu mfawidhi wa mkoa wa Mbeya.
*****
Na mwandishi wetu
Hukumu ya kesi inayomkabili mbunge wa jimbo la Mbarali Dickson Kirufi ya kutishia kuuwa kwa maneno ambayo ilitarajiwa kutolewa leo imesogezwa mbele hadi hapo vikao vya bunge la tano vitakapomalizika.

Taarifa zilizotufikia kutoka mahakamani zinadai kuwa mahakama imeumua kusogeza mbele kesi hiyo ili kumwezesha Mbunge Kirufi kuhudhuria vikao vya bunge.
Kabla ya mahakama kutoa tarehe ya hukumu Mbunge Kirufi alijitetea mahakamani hapo kuwa hausiki na kesi inayomkabili na kwamba hiyo ni njama ya baadhi ya watu wanaotaka kumwaribia kisiasa.

0 comments:
Post a Comment