Wakazi wa kata ya Iyela mtaa wa Airport wakifanya jitihada za kuokoa maisha ya Fraida Mwashozya mwenye umri wa miaka 25 mkazi wa kijiji cha Igale wilayani Mbozi, zimegongwa mwamba baada ya kufikwa na mauti wakati akichimba kisima chenye futi 96 kipenyo cha futi 2.
Mwili wa marehemu Fraida Mwashozya ambaye amefariki wakati akichimba kisima chenye kicha cha futi 96 na kipenyo cha futi mbili,
Bwana Mwanyelele ambaye alizirai wakati alipojaribu kwenda kuokoa mwili wa marehemu Fraida.
Kikosi cha Zima moto mkoani Mbeya kikitumia huduma ya hewa safi, kujaribu kunusuru kifo cha marehemu Fraida.
Na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Licha ya juhudi za wakazi wa kata ya Iyela mtaa wa Air Port jijini Mbeya kujaribu kuokoa maisha ya Fraida Mwashozya mwenye umri wa miaka 25 mkazi wa kijiji cha Igale wilayani Mbozi, zimegongwa mwamba baada ya kufikwa na mauti.
Juhudi hizo zilifikia kikomo majira ya saa 11 jioni pale mwli wake ulipoibuliwa kutoka katika kisima hicho akiwa amefariki, juhudi za uokozi zilianza majira ya asubuhi kuanzia saa moja na dakika arobaini na tano ambapo marehemu mbaye alikuwa akichimba kisima chenye urefu wa futi 96 na kipenyo cha mzunguko futi 2 kazi iliyofanyia kwa siku moja wakati akitaka kumridhisha mwajiri wake aliyemwagiza kukichimba kisima hicho.
Inaelezwa kuwa Fraida Mwashozya na mwenzake Nesco Mwamlima mwenye umri wa miaka 23 walipewa ajira ya kuchimba kisima chenye urefu wa futi 96 bwana Piusi Simchimba mwenye umri wa miaka 64 kwa ujira wa shilingi elfu 55 ambapo baada ya kumaliza waliambiwa hawatoweza kulipwa hadi watakapo ongeza urefu wa kisima hicho.
Tukio hilo la kutumbukia kwa Fraida limetokea jana majira ya saa moja za asubuhi lakini Jeshi la polisi, kikosi cha uokoaji na wakazi wa eneo hilo wameshindwa kumuokoa na kwamba jitihada za kutumia watu kuingia kisimani humo zimeshindikana kutokana na kukosekana kwa hewa kisimani humo.
Aidha watu wawili Nesco Mwamlima na Juma Mwanyeyere walipojaribu kuingia kwenye kisima hicho kumuokoa nao walishindwa kutokana na kuhishiwa hewa lakini wao waliokolewa na afya zao zinaendelea vizuri.
Afisa mtenda wa kata ya Iyela Ezekiel Kipako amesema zoezi la uokoaji limemalizika na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa mkoani Mbeya.
0 comments:
Post a Comment