Na mwandishi wetu.
Mkurugenzi wa jiji la Mbeya Juma Idi amewataka wafanyabiashara kuacha mara moja kuning’iniza bidhaa zao nje ya maduka.
Ameongeza kuwa mfanyabiashara ambaye atakamatwa akipanga bidhaa zake nje atachukuliwa atua za kisheria ikiwa ni pamoja na kutozwa faini ya shilingi elfu hamsini.
Hivi karibu halmashari ya jiji la Mbeya imefanikiwa kuwadhibiti wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama machinga kufanya biashara zao katika sehemu ambazo haziruhusi.
Machinga hao walikuwa wakipanga bidhaa zao hadi barabara hali iliyokuwa ilisababisha usumbufu kwa watenbea kwa miguu na magari kutokana na barabara kubanwa na machinga hao.
Hata hivyo masoko yaliyotengwa na halmashauri kwa ajili ya machinga kufanya biashara zao ni soko la Maendeleo, Air port, Forest pamoja na soko la Isanga.
0 comments:
Post a Comment