Pages


Home » » Mashirika ya Umoja wa mataifa yametoa shilingi milioni 303,498,000 kwa mkoa wa Mbeya ili kufanikisha chanjo ya magonjwa sugu kwa watoto

Mashirika ya Umoja wa mataifa yametoa shilingi milioni 303,498,000 kwa mkoa wa Mbeya ili kufanikisha chanjo ya magonjwa sugu kwa watoto

Kamanga na Matukio | 05:24 | 0 comments
Kaimu Mganga mkuu, Hospitali ya mkoa wa Mbeya Bi Agnes Buchwa
*****
Na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
 Mashirika ya Umoja wa mataifa yametoa shilingi milioni 303,498,000 kwa mkoa wa Mbeya ili kufanikisha chanjo ya magonjwa sugu kwa watoto kama surua, kupooza, Minyoo na Vitamini A zoezi lilokamilika kwa mafanikio.

Kaimu Mganga mkuu, Hospitali ya mkoa wa Mbeya Bi Agnes Buchwa ameyataja makundi na chanjo husika kwamba watoto 453,127 walitarajiwa kupewa chanjo hiyo kwa ajili ya surua, watoto 535,995 walitakiwa kupewa chanjo ya magonjwa ya kupooza, watoto 477,700 walipaswa kupatiwa dawa ya Vitamini A na 419,404 walitarajiwa kupewa dawa ya minyoo.

Bi Agnes amewataka wazazi kutowatuma watoto kwenye vituo vya chanjo hali inayopelekea watoto hao kutohudhuria chanjo kutokana na kuishia njiani kutokana na umbali wa kituo hadi kituo.

Fedha zimetolewa na mashirika ya WHO, UNICEF ambayo hujihusisha na masuala ya Afya na watoto duniani yanayomilikiwa na Umoja wa mataifa.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger