Pages


Home » » MKURUGENZI NA MEYA JIJI LA MBEYA KUCHUKULIWA HATUA KISA, KUWA VINARA WA VURUGU ZA MWANJELWA NA KUMSINGIZIA KANDORO.

MKURUGENZI NA MEYA JIJI LA MBEYA KUCHUKULIWA HATUA KISA, KUWA VINARA WA VURUGU ZA MWANJELWA NA KUMSINGIZIA KANDORO.

Kamanga na Matukio | 05:56 | 0 comments

MKUU WA MKOA WA MBEYA ABBAS KANDORO

* N i kutokana na kupimana nguvu za maamuzi

Na, Gordon Kalulunga, Mbeya
Maaskofu,Wachungaji na wanataaluma mkoani Mbeya wametoa tamko la kumtaka Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, kuwachukulia hatua za kinidhamu Meya wa Jiji la Mbeya, Athanas Kapunga na Mkurugenzi wa Jiji hilo Juma  Idd kutokana na kuwa chanzo cha vurugu zilizotokea jijini hapa hivi karibuni

Tamko hilo limetolewa leo katika Kongamano la kujenga mkakati wa maendeleo ya Mkoa wa Mbeya ambalo liilifanyika katika ukumbi wa Kanisa la Winners lililopo jijini hapa kutoka makanisa yote yaliyopo mkoani Mbeya ambalo Mkuu wa Mkoa alikuwa mgeni rasmi.

Mchungaji William Mwamalanga, ambaye pia ni Mkurugenizi wa taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya kuhifadhi Mazingira mkoani Mbeya (MRECA) alisema maaskofu na wachungaji wanasikitishwa na vurugu zilizotokea eneo la Mwanjelwa Jijini Mbeya na kwamba hata  Meya na Mkurugenzi wa Jiji wachukuliwe hatua za kinidhami kutokana na kuwa chanzo cha vurugu hizo.

Alisema ''Vurugu zilizotokea haikuwa ni siasa bali ni maamuzi mabaya yaliyofanywa na viongozi waAndamizi wa Jiji la Mbeya katika kushughulikia tatizo la wamachinga wanaouza bidhaa zao eneo la Mwanjelwa''
“Tukiwa na uongozi wa uongo  jiji halitasonga mbele kimaendeleo, vurugu zilizotokea kimsingi pale siyo siasa bali ni maamuzi mabaya ya baadhi ya watu, “alisema Mwamalange huku akishangiliwa na mamia ya viongozi wa dini walioshiriki kongamano hilo.

Alisema maaskofu na wachungaji wanasikitishwa na kitendo cha baadhi ya watu kumsingizia Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Kandoro kwamba yeye alikuwa ndiye chanzo cha vurugu hizo wakati siku ya tukio alikuwa katika ziara wilayani Mbozi kukagua miradi ya maendeleo.

Mchungaji Mwamalanga alisema kimsingi viongozi wa Jiji la Mbeya hasa Meya na Mkurugenzi hawawezi wakakwepa katika suala la vurugu za Mwanjelwa kwasababu walikiwa na nafasi ya kuzungumza na wamachinga kwa utaratibu ambao usingezua vurugu.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro alisema anashangaa na baadhi ya watu wanaomsingizia kwamba alishiriki kuchochea vurugu za wamachinga wakati siku vurugu zinatokea alikuwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani Mbozi na kwamba Serikali inawatambua wamachinga kama sehemu ya jamii na haiko tayari kukaa nao mbali na katika soko linalojengwa Mwanjelwa watapata nafasi.

Kandoro alisema tangu ateuliwa hajawahi kumwagiza mtu au kiongozi yeyote wa Jiji la Mbeya achukue hatua yeyote dhidi ya wamachinga na kusababisha kutokea vurugu.
“Sijawahi kumwagiza mtu achukue hatua yeyote iliyosababisha vurugu na kimsingi sina sababu maana kwanza ilikuwa ni mapema mno kuchukua maamuzi hayo maana sisi wageni unapofika katika mkoa unahitaji kwanza kusoma mkoa na siyo ghafla unaanza kuchukua hatua,”alisema Kandoro

Kandoro alisema hata hivyo Halmashauri ya Jiji la Mbeya ipo katika mpango wa kuweka utaratibu mzuri wa kuwafanya wamachinga kufanya biashara zao.

Aliongeza kuwa kinachotakiwa ni kuwajengea mazingira wamachinga kufanya biashara zao na pia kufufua viwanda vilivyosimama uzalishaji ili waweze kupata ajira katika viwanda hivyo.

Tamko hilo limekuja wiki moja tu tangu Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya kilipotoa tamko la  kuchukua maamuzi magumu ya kuwachukulia hatua kali za kinidhamu viongozi wandamizi na watendaji wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya walioshindwa kutimiza wajibu wao na kupelekea kutokea kwa vurugu zilizozua mapambana kati ya wamachinga na polisi jijini hapa.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya, Nawab Mullah alitoa tamho hilo tamko hilo kwa kusema kuwa CCM haiwezi kuacha viongozi wachache ndani ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya wawe chanzo cha vurugu hizo na kusababisha kuvunjia kwa amani kwa maslahi yao binafsi na kupelekea  wananchi kuilaumu serikali ya CCM.

“Kutokana na vurugu za Mwanjelwa CCM baada ya kutafakari kwa kina suala hili na kufanya utafiti wake wa jinsi vurugu zilivyokea na wananchi wa ndani na nje ya mkoa wanavyolizungumzia kimeazimia kuchukua hatu kali kwa viongozi na watendaji wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya walioshinda kutimiza wajibu wao,”alisema Mullah katika tamko hilo.

Mullah alisema CCM ni chama makini ambacho kinawajali na kuwapenda wananchi wake kwa hiyo italazimika kuchukua maamuzi hayo magumu kwa kuhakikisha wale wote wanaoharibu sifa ya Jiji la Mbeya wanaondolewa ili kurejesha imani ya wananchi kwa jiji na serikali ya CCM.

Alisema  wananchi lazima watambue kuwa vurugu ni kama mvua zinanyesha na kuleta mafuriko ambayo huleta madhara makubwa kwa kusomba kila kitu ambapo nchi kadhaa za Afrika zikiwemo Libya,Misri na Somalia zimeingia katika machafuko ya vita ambayo chanzo chake ni baadhi ya vyama vya siasa kutaka madaraka kwa nguvu kwa kuwashinikiza wananchi kufanya maandamano na vurugu.

Mullah alisema kwa kuwa CCM na serikali yake vipo makini kitaendelea kudumisha amani ya nchi hasa kwa kutambua kuwa hakuna nchi dunia iliyofanikiwa kujenga amani kwa kuvurugu hivyo wanaokuwa chanzo cha kutaka kuvunjika kwa amani watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Vurugu hizo za wamachinga waliokuwa wakipinga kuhamishwa maneeo yao ya kufanyiwa biashara zilianza tangu Novemba 11 mwaka huu na kudumu kwa takribani siku tatu zilisababisha kifo cha mtu mmoja, watu 17 kujeruhiwa kati yao watano kwa kupigwa risasi za moto ambapo polisi walifanikiwa kuwatia mbaroni watu zaidi ya 300 wanaosadikika kushiriki katika vurugu hizo.

Hata hivyo wamachinga hao walisitisha mapambano hayo ambayo pia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) lililazimika kuingilia kati baada ya Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi kuwasili mjini hapa akitokea mkoani Dodoma ambako alikuwa akihudhuria vikao vya bunge na kuwaomba kusitisha vurugu ambapo walimsikiliza na kuacha kuendelea na vurugu.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger