Mlemavu mmoja Bi Eliza Kahawa mwenye umri wa miaka 45 nkazi wa Mlimareli mji mdogo wa Mbalizi wilaya ya Mbeya vijijini MKoani Mbeya wamaeibiwa ng'ombe watatu usiku wa kuamkia jana.
Mlemamvu huyo alitoa taarifa katika uongozi wa kitongoji cha Mlimareli ambapo Mwenyekiti Bwana Ambonisye Masinga na mjumbe wa serikali ya mitaa Bwana Ambakisye Mwasomola waliitisha mkutano wa hadhara kuhusiana na tukio hilo na matukio mengine ambayo yamekuwa kero mtaani hapo toka Oktoba mwaka huu kwa lengo la kubaini wezi wanaohusika na matukio hayo..
Baahi ya watu wengine walioibiwa mali zao ni pamoja na Mchungaji Bahati Simbaya, ambaye aliibiwa Televisheni, Receiver pamoja na deki mwingine ni Ityana Mhindi aliibiwa baiskeli, Televisheni na Receiver, naye Bwana Isambi Mbunji aliibiwa baiskeli mbili, maharage debe kumi na tano, mahindi gunia moja na alizeti gunia moja.
Kufuatia mkutano huo kwa pamoja wananchi walifanikiwa kupiga kura ili kuwabaini wezi sugu katika mtaa huo ambapo watu watatu walipata kura za juu zaidi ambao ni Basyobile Philemon(Kasheshe) alipata kura 55, Mwamengo kura 20 na Elia Mwaigaga alijinyakulia kura 10, pia alikuwemo mtoto mdogo mwenye umri wa miaka 13 maarufu kwa jina la Wille ambaye alijizolea kura 3.
Baada zoezi la upigaji kura kukamilika watuhumiwa waliitwa kujieleza lakini Kasheshe na Mwamengo walitoroka kusikojulikana ambapo alibakia Bwana Elia Mwaigaga ambaye alikanusha tuhuma hizo nakuomba asamehewe kama alihusiwa hivyo.
Hata hivyo mkutano huo ulizaa matunda kwani ng'ombe wawili kati ya watatu walipatikana na hivyo katika juhudi za kuimarisha Ulinzi shirikishi na Usalama wa raia mikononi mwa wananchi wenyewe ambapo Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Abbas Kandoro alizindua Kamati ya mafanikio inayohusika na Ulinzi na Usalama, pia kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na dhana nzima ya kuleta amani na utulivu mkoani hapa.
0 comments:
Post a Comment