Pages


Home » » WASIFU WA MAREHEMU DAUDI MWAGOSI

WASIFU WA MAREHEMU DAUDI MWAGOSI

Kamanga na Matukio | 01:01 | 0 comments
Wasifu wa Marehemu Daudi Mwagosi

Aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha chanell Ten kituo cha Iringa aliyefariki kwa kuuawa na askari kwa kufyatiliwa kitu kinachodaiwa kuwa ni bomu Agosti 2 saa 9;30 kijijini Nyololo wilayani Mufindi.

 Alizaliwa Januari 30 1972 katika mji wa Bankroft nchini Zambia: Baba yake ni Anyingisye Mwangosi na mama yake  Bi, Kissa Myogels akiwa ni mtoto wao wa kwanza kati ya  watoto wao wawili wa pili anaitwa Anderw Mwangosi.

Elimu.
Alipata elimu ya msingi katika shule ya Chambeshi nchini Zambia ambapo alisoma hadi darasa la tatu na kuhamia nchini Tanzania wilaya ya Tukuyu kijiji cha Bsoka ambapo alimaliza darasa la saba na kufaulu kujiunga shule ya sekondari ya Tosamaganga na kusoma kidato cha kwanza hadi cha nne ambapo alijiunga na Chuo cha Uhasibu Mbeya na kumaliza diploma mwaka 1998 ambapo mwaka 2000 aliajiriwa na shirika la umeme Tanesco na kufanya kazi kwa muda wa miaka miwili tu na kuacha kazi hiyo mwaka 2002. Alianza kazi ya upigaji picha za mnato na za kutembea ambapo alihamia mkoani Iringa na kufanya kazi zake huko.

Mwaka 2002 alifanikiwa kuoa mke Bi. Itika Rauben Mwakapeje  na kufanikiwa kupata  watoto wanne wakiwemo watatu wa kiume na mmoja wa kike.

Mwaka 2005 akaanza kujihusisha na kazi ya uandishi habari kwa ushawishi wa Bw. Dominick Hule ambaye alikuwa rafiki yake wa karibu aliyekuwa akiripotia chombo cha channel ten na kumfundisha kazi hiyo ambapo uongozi uliona anafaa kufanya nae kazi wakamkubali atumikie chombo chao, na kujikita zaidi kwa kujiunga na chama cha waandishi wa habari  IPC. Mwaka 2011 alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa klamu ya waandishi wa habari Iringa IPC  na kufanya kwa uadilifu na kuongoza wanahabari mkoani humo hadi mauti yalipomkuta.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger