TAMKO LA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA MBEYA (MBPC) DHIDI YA JESHI LA POLISI NCHINI.
Chama
cha waandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya (MBPC)kimepokea kwa masikitiko
taarifa ya mauaji ya Mwandishi na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa
habari Mkoa wa Iringa, Daudi Mwangosi yanayodaiwa kufanywa na Jeshi la
Polisi Mkoani Iringa tarehe 2/9/2012.
Kutokana
na mauaji hayo na kutoridhishwa na nguvu kubwa kupita kiasi
inayotumiwa na polisi dhidi ya raia, Waandishi wa habari Mkoa wa Mbeya
wanaungana na waandishi wa habari nchini kusitisha kutoa taarifa za
jeshi la polisi hadi hapo jeshi hilo litakapokubali kuchukua hatua kali
za kinidhamu kwa polisi waliohusika kufanya mauaji hayo akiwemo,
Kamanda wa polisi Mkoa wa Iringa aliyeongoza operesheni hiyo.
Tamko
hilo pia limeeleza wazi kuwa muda umefika kuwe na mkataba maalumu wa
kazi kati ya waandishi wa habari na jeshi la polisi na kwamba
atakayekiuka hatua za kisheria dhidi ya majukumu ya kila chombo
zichukuliwe hatua kali za uwajibishaji.
Ili
kujenga dhana ya uwazi na uwajibikaji,Waandishi wa habari Mkoa wa
Mbeya wanamtaka Waziri wa mambo ya ndani, Mkuu wa jeshi la polisi
nchini (IGP) na Kamanda wa mkoa wa Iringa wajiuzulu nyadhifa zao kwa
kuwa wameshindwa kusimamia vyema usalama wa raia na mali zao.
Pia
Tamko hilo limebainisha mfumo wa uundwaji wa tume ya kuchunguza kifo
hicho haupaswi kuongozwa na Jeshi la polisi kwa kuwa ndio waliohusika na
mauaji hayo na kwamba tume huru itakayoundwa ipewe muda maalumu ili
majibu yapatikane mapema na kwa haraka na hatua za kisheria zichukuliwe
kwa wahusika.
Waandishi
wa habari Mkoa wa Mbeya, wanaamini kuwa Serikali na jeshi la polisi
litachukua hatua stahiki kwa waliohusika na mauaji ya Mwandishi Daudi
Mwangosi, na pia Polisi watajitathmini upya katika utendaji wa shughuli
zake hasa katika udhibiti wa vurugu na uzuiaji wa maandamano.
………………………………..
Christopher Nyenyembe,
Mwenyekiti MBPC.
Nakala ;
1.Mkuu wa Mkoa wa Mbeya na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama.
2.Inspekta wa Jeshi la Polisi(IGP).
3.Vyombo vyote vya Habari.
0 comments:
Post a Comment