*Kichwa chake chapasuka na utumbo watoka nje.
Habari na Ezekiel Kamanga,Sumbawanga Vijijini.
Mwanafunzi
wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Kilangawana,Kijiji cha
Maleza,Kata ya Kapeta,Wilaya ya Sumbawanga Vijijini Mkoani Rukwa aitwaye
Imani Nzala(12),amefariki dunia baada ya kudondokewa na mti ulikokuwa
ukikatwa na Babu yake Bwana Nzala kwa ajili ya kuchomea tanuli la
tofali.
Katika
ajali hiyo ya kusikitisha iliyotokea Septemba 16 mwaka huu majira ya
saa tano,mtoto huyo alipasuka kichwa na utumbo wake kutoka nje hali
iliyopelekea kukimbizwa hadi Kituo cha Afya cha Kilangawana.
Licha
ya marehemu kukimbizwa katika kituo hicho akiwa bado hajafariki,Muuguzi
wa kituo hicho aliomba Imani awaishwe hadi Kituo cha Afya cha
Kamsamba,ambako huko kutokana na tatizo hilo kuwa kubwa waliomba
asafirishwe hadi Hospitali ya Wilaya ya Mbozi,lakini kabla ya gari la
wagonjwa kufika mwanafunzi huyo alifarikia dunia.
Hata
hivyo Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Kamsamba Bwana Michael
Kajemi,amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba kifo cha
mwanafunzi huyo kimetokana na kuvuja damu nyingi katika mwili wake.
Mazishi ya kuupumzisha mwili wa marehemu Imani,kwenye nyumba yake ya milele yamefanyika Septemba 17 mwaka huu kijijini kwao.
0 comments:
Post a Comment