Na
Ezekiel Kamanga,Mbeya
Ajuza
mwenye umri wa miaka 80 aliyefahamika kwa jina la Bi. Janeth Nenje, amenusurika
kifo baada ya kucharangwa na mapanga na mtu aliyefahamika kwa jina la Pato
Lwiza Mkazi wa Kitongoji cha Chang'ombe,Kijiji cha Mbuyuni Wilaya ya Chunya
Mkoani Mbeya.
Tukio
hilo la kusikitisha limetokea kijijini hapo Septemba 19 mwaka huu majira ya saa
mbili usiku ambapo mtuhumiwa alimfuata ajuza huyo nyumbani kwake na kuanza
kumcharanga kwa mapanga na kisha kumjeruhi vibaya hali iliyopelekea kukimbizwa
katika Kituo cha Afya kilichopo kijijini hapo.
Imedaiwa
kuwa siku za hivi karibuni mtuhumiwa Bwana Lwiza alimtuhumu ajuza huyo kuwa ni
mshirikina hali iliyomfanya kuingiwa na hasira na kumtendea ukatili huo sehemu
mbalimbali za mwili wake.
Aidha
Bi. Nenje hivi sasa amelazwa katika kituo hicho cha afya cha Mbuyuni na hali
inaendelea vema.
Baada
ya msako mkali wananchi walifanikiwa kumkamata Bwana Lwiza na kuanza kumsulubu
kabla ya kuokolewa na Afisa Mtendaji wa Kijiji Bwana Mwashiuya kwa kushirikiana
na Mgambo wa Kijij hicho kabla ya kukabidhiwa mikononi mwa polisi wa Kituo cha
Mkwajuni.
Katika
tukio jingine Mwananchi mmoja Mkazi wa Kijiji cha Lulasi,Kata ya Mpombo Wilaya
ya Rungwe Mkoani hapa ameuawa na mtu au watu wasiuofahamika kisha kutumbukizwa
katika Kisima cha Maji safi kinachomilikiwa na mmoja wa wakazi wa kijiji hicho.
Tukio
hilo limegunduliwa na wananchi wa kijiji hicho waliokuwa wakiteka maji katika
kisima hicho na kubaini harufu kali katika maji hayo yanayotumika katika
matumizi ya nyumbani kama vile kunywa,kupikia na kufulia.
Hali
ilizidi kuwa mbaya Septemba 22 mwaka huu majira ya saa 8 mchana baada ya
wananchi kadhaa waliokuwa wakiteka maji hayo kuambua kukivunja kisima hicho
kinachomilikiwa na Bwana Noah Mwambalaswa na kuukuta mwili wa marehemu ukiwqa
kichwa chini miguu juu,hivyo taarifa kutolewa kwa viongozi wa kijiji hicho.
Mwenyekiti
wa Kijiji hicho Bwana Jimmy Mwalupaso amethibitisha kutokea kwa tukio hilo
ambapo Daktari wa Hospitali ya Wilaya hiyo alifika eneo la tukio na kuufanyia
uchunguzi mwili wa marehemu na kubaini kuwa alipingwa na kitu
kizito(nondo) kichwani hali iliyompelea marehemu kuvuja damu nyingi mpaka mauti
yalipomfika.
Hata
hivyo baada ya uchunguzi wa daktari mwili wa marehemu ulikabidhiwa kwa ndugu wa
marehemu kwa ajili ya mazishi yaliyofanyika kijijini hapo Septemba 23 mwaka
huu.
0 comments:
Post a Comment